FURAHA YA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna pande mbili za kazi ya Kristo pale Kalvari. Upande mmoja ni kwa manufaa ya mwanadamu, na upande mwingine ni kwa manufaa ya Mungu. Mmoja humnufaisha mwenye dhambi, na mwingine humnufaisha Baba.

Tunafahamu vyema faida kwa upande wa binadamu. Msalaba wa Kristo umetupatia msamaha wa dhambi zetu. Tumepewa uwezo wa ushindi juu ya vifungo vyote na mamlaka juu ya dhambi. Tumepewa rehema na neema. Bila shaka, tumepewa ahadi ya uzima wa milele. Msalaba umetupa njia ya kutoroka kutoka kwa hofu ya dhambi na kuzimu.

Ninamshukuru Mungu kwa faida hii ya msalaba kwa wanadamu na kwa unafuu wa ajabu unaoleta. Ninafurahi kwamba inahubiriwa wiki baada ya juma katika makanisa ulimwenguni kote.

Bado kuna faida nyingine ya msalaba, ambayo tunajua kidogo sana kuihusu. Hii ni kwa faida kwa Baba. Tunaelewa kidogo sana kuhusu furaha ya Baba ambayo iliwezeshwa na msalaba. Ni furaha inayomjia kila anapopokea mtoto mpotevu ndani ya nyumba yake.

Kwa maoni yangu, Wakristo wengi wamejifunza kuja kwa ujasiri mbele za Mungu kwa ajili ya msamaha, ugavi wa mahitaji na majibu kwa maombi; lakini wanakosa ujasiri katika kipengele hiki cha imani, kipengele ambacho ni muhimu vivyo hivyo katika kutembea kwao na Bwana.

Ndio maana maandiko yanasema, “Basi, ndugu, kwa kuwa na ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, kwa njia ile aliyoiweka wakfu kwa ajili yetu mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake. Na tukaribie wenye moyo wa kweli, katika utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi” (Waebrania 10:19-20, 22).

Ikiwa yote tunayozingatia kuhusu msalaba ni msamaha, tunakosa ukweli muhimu ambao Mungu amekusudia kwetu kuhusu msalaba. Kuna ufahamu kamili zaidi wa kuwa hapa, na unahusiana na furaha yake. Kweli hiyo huwapa watu wa Mungu mengi zaidi ya kitulizo tu. Inaleta uhuru, pumziko, amani na furaha.