Uwezo Wake wa Kutoa

David Wilkerson (1931-2011)

Jeshi la Ashuru lilipozunguka Yerusalemu, Mfalme Hezekia aliamua kutoegemea mkono wa nyama bali kumtegemea Mungu.

Mfalme alijinyenyekeza na kumtafuta Mungu katika maombi. “Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alirarua mavazi yake, akajivika nguo ya magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA” (Isaya 37:1). Hezekia alikiri, “Bwana, najua sina kitu cha kukupa isipokuwa imani yangu. Sina uwezo wa kupigana na Senakeribu. Tumezungukwa na maadui zetu. Tafadhali, tupe mwelekeo wako!”

Hezekia alijua kwamba Isaya angepewa mwongozo wa neno la Mungu, kwa hiyo wakati huu alimtuma mjumbe wake kwa nabii huyo. Watu hawa walimwambia Isaya, “Siku hii ni siku ya dhiki, na karipio, na matukano; kwa maana watoto wamezaa, lakini hapana nguvu za kuwazaa” (Isaya 37:3). Kwa maneno mengine, walikuwa wakisema, “Wakati huu, tunataka kufanya kila kitu kwa njia ya Mungu, lakini hatuna nguvu iliyobaki. Tufanye nini?”

Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu hivi, Bwana asema hivi, Usiogope maneno hayo uliyoyasikia; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe. (Isaya 37:6-7).

Mungu alikuwa akisema, “Adui wenu yeyote ni adui yangu kwa sababu mmenikabidhi vita. Nitamshughulikia adui huyo, awe ni mwanadamu au ni shetani.”

“Hataingia ndani ya mji huu, wala hatapiga mshale huko, wala hataukaribia kwa ngao, wala hatajenga boma la kuuhusuru” (Isaya 3:33). Hata kama wengine wanaweza kuwa karibu nawe, hiyo haimaanishi chochote. Unapotembea katika agano na Mungu, anaahidi kufanya vita dhidi ya kila adui anayekushambulia.

Ni picha nzuri sana ambayo Mungu ametoa kuhusu uwezo wake wa kutukomboa kutoka kwa adui zetu. Adui anaweza kutupa mishale yenye moto, lakini hawatapiga. Shetani anaweza kutushambulia kwa kelele na jeshi kubwa la tamaa na majaribu, lakini mwisho, atageuka na kukimbia. Mungu amesema, “Nitamlinda kila mtoto wangu aniaminiye hata kuuweka upanga wake mwenyewe.”

 
Child smiling - More Hope in 2025

You Can Bring Real Hope

 

In 2024 millions have been ministered to online. Thousands of disciples have been made. Hundreds of churches have been planted. Dozens of communities have been transformed both spiritually and physically. This is the power of the gospel at work through your financial partnership with World Challenge.