Kumiminiwa kwa Roho Wake

Gary Wilkerson

Baadhi ya Wakristo wanadai, “Kila kizazi kina wahubiri wa siku ya maangamizi. Sikuzote wamesema, ‘Huu ndio wakati mbaya zaidi katika historia.’ Lakini Shetani anaendelea kumwaga uovu. Yeye haachi kamwe.”

Ni kweli kwamba shetani hajabadilisha mbinu zake. Tofauti yake leo ni kupata wingi wa masikio yenye usikivu zaidi. Kadiri anavyopata msingi mkubwa, ndivyo anavyotafuta kudai zaidi. Anachochea fikra potovu zaidi, akiwahimiza wale wanaompinga Mungu, “Haitoshi. Unataka zaidi!”

Tafadhali elewa kuwa watu wenye akili nyeusi sio adui zetu. Hatupaswi kuwahukumu wale wanaofuata mtindo wa maisha tofauti na wetu. Tunapaswa kuwapenda kwa upendo ambao tumeonyeshwa na Yesu, kuwaletea habari njema zilezile tunazohitaji kama watenda-dhambi wenzetu wanaohitaji msamaha na wokovu.

Kwa Roho Mtakatifu, ninaona sisi tukizamisha kilio cha ulimwengu na kilio chetu, “Haitoshi! Lazima kuwe na Roho wa Mungu zaidi mioyoni mwetu, ujasiri zaidi wa kuhubiri habari njema zake, uadilifu zaidi wa kutetea haki, nguvu zaidi za kuvunja mshiko wa Shetani juu ya kila moyo anaotawala.”

Katika wakati ambapo Shetani ametia giza akilini kwa udanganyifu mbaya, tutaona ushuhuda ukiinuka. Kila moyo wenye njaa ya haki, ukipanda machozi juu ya ulimwengu uliovunjika, utalishwa na Bwana mwenyewe. Atajaza akili zetu na maono ya utukufu na vinywa vyetu na maneno ya kinabii ambayo hatukuwahi kufikiria kuwa tunaweza kusema. “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; wana wenu na binti zenu watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono” (Yoeli 2:28).

Je, utaichochea roho yako kumtafuta Mungu kwa Roho wake zaidi, machozi zaidi juu ya ulimwengu uliovunjika, njaa zaidi ya kumwona Yesu akitenda kazi kupitia kwako? Nataka kuwa mmoja anayesema, “Ninachokiona leo hakitoshi. Nijaze, Bwana, nitumie, fanya kazi ndani yangu niufanye ufalme wako kwa ajili ya jina lako.” Ninaamini utaungana nami katika kusihi kumwagwa kwa Roho wake kuliko hapo awali. Amina!

 
Child smiling - More Hope in 2025

You Can Bring Real Hope

 

In 2024 millions have been ministered to online. Thousands of disciples have been made. Hundreds of churches have been planted. Dozens of communities have been transformed both spiritually and physically. This is the power of the gospel at work through your financial partnership with World Challenge.