Kusimama kwenye Ahadi Yake.

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu hutia muhuri ahadi zake zote kwa kiapo, na tuna haki “ya kisheria” ya kusimama juu yake. Mungu hawezi kughairi ahadi zake zozote, au hangekuwa Mungu. Tunaweza kushikilia kila ahadi na kutangaza, “Bwana, nitasimama juu ya yale uliyosema.”

Hii haimaanishi kuwa hatutakiwi kuwasiliana na Bwana, lakini ushirika wetu hauzuiliwi tu kuabudu, kusifu au kusali. Tunawasiliana naye kwa kuegemea kikamilifu Neno Lake lililoandikwa na kufunuliwa, na ushirika wetu pamoja naye pia unatia ndani kumwamini.

Roho Mtakatifu "huzungumza" zaidi kwa kutuongoza kwa vifungu muhimu vya maandiko, akituonyesha mawazo ya Mungu juu ya jambo lolote, na kutuambia ni hatua gani za kuchukua. Kwa nini aongee kwa sauti ya ndani wakati “hatutasikia” sauti yake iliyofunuliwa na iliyoandikwa?

Si lazima Mungu atuambie kila kitu au kutufunulia mipango yake yote. Tunaweza kuwa na urafiki wa karibu pamoja na Mungu kwa kuacha tu jitihada zetu za kujua sauti yake. Urafiki wa aina hii unasema, “Bwana, hata kama sitawahi kusikia neno lingine kutoka kwako, najua bado unatoa kila kitu ninachohitaji. Unanipenda, Neno lako ni kwa ajili yangu, nami nitapumzika katika hilo.”

Daudi ni mfano wa aina hii ya uaminifu. Mtu huyu mcha Mungu alipokuwa amelala kwenye kitanda chake cha kufa, alisema, “Ijapokuwa nyumba yangu si hivyo kwa Mungu, lakini amefanya nami agano la milele, lililoamriwa katika mambo yote, lililo salama…” (2 Samweli 23:5). Kwa maneno mengine, Daudi alikuwa bado hajaona utimizo wa maneno yote ya Mungu, hata hivyo alipewa ahadi kwamba nyumba yake haitaanguka.

Daudi hakuwa na nabii aliyemwambia mambo haya, wala hakuwa na ndoto, maono, au sauti ya ndani ikizungumza naye. Badala yake, alipokabiliana na umilele, alisema, “Mungu alinipa ahadi ya agano katika Neno Lake, nami nitaingia katika umilele nikisimama juu ya ahadi hiyo.” Daudi aliendelea katika mstari uleule: “Kwa maana huu ndio wokovu wangu wote, na shauku yangu yote” (2 Samweli 23:5). Kimsingi, alikuwa akisema, “Ninaweza kukabiliana na kifo sasa kwa sababu ahadi yake ndiyo tu ninayohitaji.”

Tunaweza kushindwa katika utambuzi wetu, kusikia, na maamuzi; lakini tunaweza kushangilia katika Mungu wetu, ambaye ni nguvu zetu. Ni lazima tu kukubali, kusimama tuli na kuona wokovu wake!

 
Child smiling - More Hope in 2025

You Can Bring Real Hope

 

In 2024 millions have been ministered to online. Thousands of disciples have been made. Hundreds of churches have been planted. Dozens of communities have been transformed both spiritually and physically. This is the power of the gospel at work through your financial partnership with World Challenge.