NEEMA NA AMANI KWENU

David Wilkerson (1931-2011)

Ninaamini kuwa maombi yaliyochanganyikana na imani ndiyo jibu la kila kitu. Paulo alisema, “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6).

“Katika kila jambo” maana yake ni “Sali juu ya kila jambo, na shukuru kwamba maombi yako yatasikiwa na kujibiwa.” Tumeambiwa tuombe kama chaguo letu la kwanza, sio baada ya kujaribu kila kitu bila mafanikio. “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa” (Mathayo 6:33).

Wakristo wengi sana leo wanatekwa nyara na Shetani. Nyumba zao zimo katika msukosuko; wanasumbuliwa na hofu na hatia; wanakabiliwa na matatizo kila upande. Matatizo ambayo huduma yetu husoma katika barua kutoka kwa Wakristo ni nyingi sana.

Hata hivyo, ili kuwa wakweli, ni waamini wachache wanaokabili matatizo wanaomgeukia Bwana kwa maombi ya bidii. Wachache leo wana muda thabiti, wa ubora pekee na Mungu katika maombi. Kukata tamaa kunaingia kwa sababu hawaendi mahali pa siri, ili kufungua roho zao na kumlilia Bwana huzuni zao. Badala yake, wanaeleza matatizo yao yote kwa marafiki, wachungaji, washauri; na wanampuuza Bwana anayengoja kuwa nao wote peke yao. Tunaomba kama hatua ya mwisho.

Je, Mungu angeweza kuhuzunishwa na kizazi hiki jinsi alivyokuwa na Israeli? Alisema juu yao, “Watu wangu wamenisahau siku zisizo na hesabu” (Yeremia 2:32).

Mungu hupendezwa tunapomkimbilia kwanza, tunapojitengenezea wakati maalum wa kuwa peke yake, kumimina hisia zetu za ndani kabisa na kuweka maombi yetu mbele zake. Hatuna haki ya kusema tunampenda Bwana ikiwa hatutumii wakati pamoja naye mara kwa mara. Atasikia maombi yako na kujibu, lakini anakuhitaji peke yako ili aweze kuzungumza nawe kwa utulivu.

Ninapoingia katika uwepo mtakatifu wa Bwana kila siku, ombi langu thabiti zaidi ni kwamba Roho Mtakatifu anifungulie Neno la Mungu ili niwe mhubiri wa kweli kwake. Na utengeneze wakati mzuri kwa ajili yake, ukimtumaini na maombi yako.