NI MSIMU WA KUTIA MOYO

Carter Conlon

Katika msimu huu, tunaona watu wengi, vijana hasa, ambao wamekata tamaa na kupoteza matumaini. Hawaoni sababu ya kuendelea kuishi; hawaoni kusudi la wakati ujao, na kwa kweli ni mojawapo ya misiba ya ki-siku-hizi ya nyakati zetu.

Ukigeukia injili ya Luka, inazungumzia jinsi Mungu alikuja kwa kila mmoja wetu. Malaika walitangaza kuzaliwa kwa Kristo kwa wachungaji, na kisha “ghafla palikuwa pamoja na huyo malaika umati wa jeshi la mbinguni wakimsifu Mungu na kusema: ‘Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na duniani amani, nia njema kwa wanadamu.” ( Luka 2:15; 13-14). Fikiria kuhusu hili kwa muda! Mungu aliyetuumba sisi na ulimwengu, ambaye angeweza kuharibu yote kwa mawazo ya akili yake; lakini anafanya nini kwa uwezo wake wote, utukufu na haki? Anashuka duniani, kwenye mji mdogo uitwao Bethlehemu, kwa sababu hakuwa tayari kuharibu uumbaji wake.

Yesu mwenyewe alisema hivi. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Ni nani angeweza kumkomboa Paulo kutoka katika mwili wake wa kifo? Ni nani angeweza kumkomboa Eliya kutoka katika hali yake ya kukata tamaa na kutamani kufa?

Wakati fulani tunasonga mbele, ingawa; hatuchukui maisha tu siku baada ya siku na kuomba nguvu za kukabiliana na siku hii. Hata hivyo, Mungu hutembea pamoja na wale wanaotembea pamoja naye. Anatupa nguvu na riziki, nasi tunakuwa kiumbe kipya.

Hatuwi watu wa dini; tunakuwa mtu mpya. Ni wangapi kati yenu ni watu tofauti na mlivyokuwa hata mwaka mmoja uliopita? Unaishi katika miujiza sasa. Najua sisimami hapa kwa uwezo wowote wa asili. Najua ninasimama na kitu ambacho Mungu alinipa nilipochagua kutembea naye. Hakuna kikomo kwa kile kinachoweza kufanywa au kuvumiliwa wakati Mungu yuko katikati ya maisha yetu.

Huu sio msimu wa kukata tamaa ukimjua Mungu au hata ukitaka kumjua Mungu. Huu ni msimu wa furaha ambao hakuna mtu anayeweza kuzungumza kutoka kwetu ikiwa tunajikabidhi kwa Kristo! Ndiyo sababu malaika waliimba ‘Shangwe kwa ulimwengu!’ Tuna amani pamoja na Mungu.

Carter Conlon alijiunga na wachungaji wa Kanisa la Times Square mwaka wa 1994 na aliteuliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka wa 2001. Mnamo Mei 2020 alibadili jukumu na kuendelea kama Mwangalizi Mkuu wa Kanisa laTimes Square Church, Inc.