Simama na Usubiri

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu anazungumza na watu wake kwa sauti ya Roho wake: “Masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni, kila mgeukapo kwenda mkono wa kuume, au mgeukapo kwenda kushoto” (Isaya 30:21).

Sauti ya Roho wake hutujia hasa kupitia maandiko. Anaweza kufungua kifungu cha kibiblia ambacho kitakuwa ufunguo wa ukombozi wetu. Hata hivyo, kabla ya kusikia sauti yake ya mwongozo, Mungu anataka tufanye jambo fulani. Tunapaswa kusimama tuli na kusubiri achukue hatua. Neno hili si pendekezo bali ni amri. Ni siri ya ushindi wetu kamili na ukombozi. Hakika, Bwana aliamuru watu wake kusimama tuli mara nyingi.

Katika Yoshua 3, tunasoma juu ya kuvuka kwingine Israeli ilibidi kufanya kwenye Mto Yordani. Mungu aliwaagiza watu hivi: “Utawaamuru makuhani waliolichukua sanduku la agano, ukisema, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, msimame katika Yordani.” (Yoshua 3:8) Mungu aliwaambia hivi makuhani waliolichukua sanduku la agano. . Kisha Mwenyezi-Mungu akaongeza, “Mara tu nyayo za makuhani wanaolichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu wa dunia yote, zitakapotulia katika maji ya Yordani, na maji ya Yordani yatakatiliwa mbali. … nao watasimama kama chungu” (Yoshua 3:13).

Mungu alisema, “Utakapofika kwenye maji, panda miguu yako ndani yake na usimame pale. Tulia, pumzika. Ngoja tu nichukue hatua, nami nitagawanya maji kwa ajili yako!”

Maneno ya Kiebrania ya kusimama tuli katika kifungu hiki yanamaanisha “komesha shughuli zote, acheni kushindana.” Ni Waisraeli wangapi walitii walipofika Yordani? Waliposimama na miguu yao ndani ya maji, wengi lazima walifikiri, "Tunajuaje kwamba hii itafanya kazi?" Huenda wengine walijaribiwa kujenga aina fulani ya daraja la pantoni ili kujaribu kuvuka kwa werevu wao wenyewe, lakini hilo lingekuwa bure.

Mungu alitenda katika tukio hilo. Aligawanya maji kwa sababu tendo la utii la Israeli liliambatana na imani. Mungu alijibu imani yao! Wapendwa, kwa imani, tukisikiliza sauti yake na kutii, yeye hutoa jibu.