DHAMBI AMBAZO MUNGU AMECHAGUA KUSAHAU

Nicky Cruz

Shetani anaishi katika siku za nyuma. Yeye ni mkuu wa vile alivyokuwa mbele, mfalme wa majuto na hatia. Anaishi ili atuweke huko, kutukumbusha yale tuliyoyafanya na jinsi ubaa tiliwoishi. Hisiya yake inem na mawazo ya ushindi wa zamani; ya nyakati ambazo alitufanya sisi kutenda dhambi, kutupa, kuanguka kwa ajili ya uongo wake. Kwa sababu katika moyo wake anajua kwamba ndivyo alivyokuwa zamani.

Wakati wokovu unakuja, vilivyo shikiliwa na Shetani vimekisha na tumaini lake la pekee ni kutufanya sisi tufikiri kama bado tunafungwa. Yeye hawezi tena kuwa na roho zetu, lakini anaweza kutufanya kuwa na mashaka na kijiona kama hatufai kuwa watoto wa Mungu.

Usimruhusu kufanya hilo. Usimruhusu ajaze akili yako mashaka na kuchanganyikiwa, na mawazo ya dhambi za zamani - dhambi ambazo Mungu amechagua kusahau. Dhambi tunazohitaji kusahau kabla tuweze kuendelea mbele.

Haitoshi kwamba tunakubali Yesu na kumwomba msamaha wake; tunapaswa pia kukataa mambo ambao tulikuwa tunaishi mbele ili tukumbatie kabisa siku mpya - siku ya wokovu wetu. Siku ya moyo mpya, akili, na nafsi mpya.

Ni muhimu kutambua kwamba kuna tofauti kubwa kati ya wingi wa watu ambao wanamfuata Kristo na wale wafuasi wachache wanaoishi kila siku na shauku kali kwa Yesu! Wamefanya zaidi kuliko kukubali wokovu; wamekubali baadaye mapema kabisa. Wamechagua kusamehe wenyewe na kuangalia mbele.

"Ndugu zangu, mimi sijihesabu kwamba nimekwisha kushikwa; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yalio nyuma, nikiyachuchumulia yaliyo mbele; nakaza mwendo, nifikilie mede ya dhawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu" (Wafilipi 3:13-14).

Usimruhusu Shetani kujaza akili yako kwa shaka na kuchanganyikiwa, na mawazo ya dhambi za zamani - dhambi ambazo Mungu amechagua kusahau. Anakupa moyo mpya, ambao haukumbuki yaliopita, atakupa tu baadaye unao angaa na wenye utukufu.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza  ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka ( Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).