DHAMBI YA KUTOAMINI

David Wilkerson (1931-2011)

Kutoamini kunahuzunisha moyo wa Mungu kuliko dhambi nyingine yoyote. Sisi Wakristo tunalia dhidi ya dhambi za mwili, lakini Mungu anahusika na dhambi za moyo - kuwa na mashaka juu ya Neno lake au kuwa na maswali juu ya uaminifu wake. Masuala halisi ya maisha na kifo ni mengi zaidi na jinsi mtu anavyofikiri kuliko kile anachofanya.

Nimewajua Wakristo ambao wanaacha dhambi zote za mwili wanazoweza kuzifikiria lakini licha ya "kusafisha tendo lao," bado hawawezi kupumzika na wasiotosheka. Kwakufanya hayo kimakosa walifikiri Mungu angefurahi kama waliacha dhambi zao za siri, kwamba baraka zitatoka moja kwa moja. Lakini dhambi za mwili ni sehemu tu ya tatizo. Walijifunza tu kumcha Bwana lakini si kumtumaini, na hofu ya kirasiku karibu huzaa kutokuamini.

Kupitia Neno lake Mungu ametoa njia ya uhakika ya kuwa na imani kamili ndani yake.

"Ulalapo hutaona hofu; naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafla, wala uharibifu wa waovu utapofika. Kwakuwa Bwana atakuwa tumaini lako, naye atakurinda mguwu wako usinaswe" (Mithali 3:24-26).

"Basi msitupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu" (Waebrania 10:35).

"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nakama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja turizomwomba" (1 Yohana 5:14-15).

Hizi ni ahadi za ajabu kutoka kwa Baba yetu wa mbinguni. Usiwe na hofu au shaka! Shughulika na kutokuamini kama ungekuwa na dhambi nyingine yoyote mbaya zaidi. Elekeza moyo wako kwa kumtegemea Bwana - na kukumbuka maneno ya Mtunga Zaburi: "Hataogopa habari mbaya; moyo wake u imara ukimutumaini Bwana. Moyo wake umethibitika hataogopa" (Zaburi 112:7-8).