FARAJA KUTOKA KWA MUNGU KATIKA MAJARIBIO
Mojawapo ya huduma zinazohitajika sana katika Kanisa la leo ni ile ya faraja - kuwafariji wengine wakati wa shida na taabu. Waumini wengi hawajui mahali pa kugeukia wanapoumia.
Mtume Paulo alikuwa mtumishi mtauwa wa Mungu aliyemtumikia Mungu zaidi humu duniani Hata hivyo.alivumilia mateso makali na ya kupindukia hata asijue la kusema. Kwa kweli, wakati mwingine alikuwa amevunjika moyo kiasi kwamba alifikiri kifo chake kilikuwa kimemfikia Hata hivyo alimwita Baba yetu wa mbinguni kuwa "Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote" (2 Wakorintho 1:3). Alisema zaidi katika sura ile ile, "Tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi" (1:8).
Kwa kumtaja Mungu kama "Baba wa rehema," Paulo alikuwa akionyesha kwamba alikuwa amejifunza kutokana na mateso yake. Aliweza hata kushangilia katika taabu zake zote kwa sababu alijua kuwa ilikuwa aina ya shule kwa ajili yake. Alijifunza kusema, "Mungu ana lengo katika hili! Watu watahitaji ushawishi wangu, faraja yangu." Katika mateso yake, Paulo alikuwa amejifunza somo muhimu la kupokea faraja ku toka kwa Bwana.
Unapoteseka ndani ya mwili wako, unakuwa mvumilivu sana na wengine ambao wanateseka. Unapata huruma mpya kwa wengine. Unaposumbuliwa na bado unampenda Bwana sana (na sio kuficha dhambi), hutaangalia mateso ya mwingine na kujiuliza, "Kwani huyu alifanya nini ili kustahili yaliyomfika?”
Watu ambao wamevumilia mateso na kuyapitia wakisalia kuwa waaminifu kwa Mungu huibuka wakiwa na nguvu, watulivu na wenye subira. Pia wana upole wa Kristo. Ni jambo la kutia moyo kuwa karibu na watu kama hawa!
Ikiwa unateseka, mtumaini Mungu kukupitisha katika mateso hayo Watu watakuona ukipata ushindi na faraja kupitia kwa nguvu za Mungu pekee na watavutiwa na kile ulicho nacho.