FARAJA KWA MIOYO YETU YENYE HOFU

David Wilkerson (1931-2011)

Maisha ya Kikristo sio maisha yenye safari ya wazi kila wakati. Kila mwamini lazima apitie siku mbaya, bila kujali kwamba ni mtakatifu. Kwa kushukuru, Wakristo wengi wanatambua kwamba Yesu hayupo tu wakati mambo yanaendelea vizuri, lakini pia yupo na wakati wa magumu. Yeye ni mwaminifu na mwenye kujali kwa kila msimu na anaguswa na kila hisia tunayopitia.

Mtume Paulo alikumbwa na siku mbaya wakati alikua akienda Makedonia. "Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu." (2 Wakorintho 7:5). Mwanamume huyu mwenye kumcha Mungu alikiri kwamba mtu wake wa ndani alikuwa na shida nyingi.

Paulo hakukuwa binadamu asio wakawayida, na alikuwa chini ya hisia za kibinadamu kama sisi. Lakini alikuwa na nidhamu na kamwe hakuzipa ndani hisia zake na majaribu yaliyokuwa anawashindikiza pamoja nao. Alishuhudia, "Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nmejaa furaha ya kupita kiasi" (2 Wakorintho 7:4).

Je! Unapitia siku mbaya, wiki mbaya, msimu mrefu wa kukata tamaa? Je, unaangushwa chini, umevunjika moyo, na mawazo ya ndani ndani? Ikiwa ndivyo, unashangaa jinsi Mungu atakavyotenda kuhusu jaribio lako? Je, atakukemea au atakuaadhibu? Hapana kamwe! Paulo anakuambia kuwa Bwana hajakuwa kamwe karibu sana na wewe, kamwe kuwa tayari kukusaidia, kuliko wakati wewe uliangushwa chini na kuumizwa.

"Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yoye; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu" (2 Wakorintho 1:3-4).

Nadhani siku zetu mbaya mara nyingi zina maana ya kutuleta katika ukomavu. Unapoendelea kutembea na Bwana, unapaswa kuwa na ufahamu zaidi kuwa una rasilimali zote zinazohitajika ili ukabiliane na adui.