FUNGA MLANGO
Katikati ya muda wa kuchangamka na machafuko, watu wa Mungu wanajibuje? Ikiwa umemkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, hauhitaji kamwe hofu. Wale ambao wako ndani ya Kristo wanahifadhiwa milele na damu ambayo Yesu alimwanga kwa ajili yao na ukweli huu ni jiwe kuu la imani yetu. Itaamua kila kitu tunachofikiri na kila tunachofanya bila kujali kinachoendelea kote kwetu.
Paulo aliwahakikishia waamini huko Roma, "Bali Mungu anaonyesha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa kuwa wakati tulikuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. Basi Zaidi sana tukisha kuhesabiwa haki na damu Yake, tutaokolewa kutoka ghadhabu kupitia Kwake" (Warumi 5:8-9).
Watu wa Mungu wanapaswa kufanya nini wakati dunia inakabiliwa na habari mbaya? Wakati masoko yanapanda na kuanguka na dunia inakuwa imepooza na hofu? Mungu huwapa watoto wake mahali pa kujificha: "Njoni, watu wangu, ingieni ndani ya vyumba vyenu, na mufunge milango yenu nyuma yenu mujifiche wenyewe kwa muda kidogo, mpaka hasira itakapopita" (Isaya 26:20).
Unapofadhaika - unapozidiwa, unapopigwa chini na maumivu, ukijali juu ya wakati ujao - Mungu anasema kuna nafasi ya faraja ambapo tunapata utulivu kwa roho zetu. Nafasi hii ya mafichoni ya siri katika akili yako ambayo Isaya anaelezea hivi: "[Bwana] atamlinda yeye ambaye moyo wake umemtegemeya katika Amani kamilifu, kwa kuwa anakuamini" (Isaya 26:3).
Wakati Bwana anatuambia, "Funga mlango," anatuonyesha haja ya kuzima sauti nyingi za shida katika vichwa vyetu. Tunapaswa kufunga mlango wa mawazo yote kuhusu kesho na kuhusu matukio ya ulimwengu. Bwana ambaye ametuleta kwa uaminifu hivi sasa hatatuacha tushindwe katika siku zijazo.
Mungu atukuzwe! Yeye ni makao yetu ya kujificha wakati wa mgogoro, na ahadi zake za uaminifu ni ngao yetu ya ulinzi. Shikamana nazo!