FURAHA YA KUTAFUTA USO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

"Neno moja nimelitaka kwa Bwana, nalo ndilo nitalolitafuta, nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana, nakutafakari hekaruni mwake" (Zaburi 27:4).

Daudi anashuhudia, "Nina sala moja, Bwana, ombi moja. Ni lengo langu moja muhimu zaidi katika maisha; linanitumia mimi na nitalitafuta kwa kila kitu kilicho ndani yangu. "Usifanye makosa, Daudi hakuwa mwenye kujipenda, akiangaa katika ulimwengu wa nje, pengine na kujificha mahali penye jangwa. Hapana, Daudi alikuwa mtu mwenye shauku wa kutenda kazi, shujaa mkuu, akiimba kwa wingi wa kushinda kwake katika vita. Pia alikuwa na shauku katika sala yake na kujitolea, kwa moyo uliotamani baada ya Mungu. Bwana alikuwa amebariki Daudi kwa matumaini mengi ya moyo wake na alikuwa amekwisha kunusa kila kitu ambacho mtu angeweza kutaka katika maisha: utajiri, nguvu na mamlaka, heshima na kusemwa vizuli. Juu ya yote haya, alikuwa akizungukwa na wanaume waliojitolea ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili yake.

Zaidi ya yote, Daudi alikuwa muimbaji, mtu mwenye kusifu ambaye alishukuru Mungu kwa baraka zake zote. Wakati Daudi aliomba ili aweze kukaa katika nyumba ya Bwana siku zote za maisha yake, hakuwa akizungumzia juu ya kuondoka kiti chake ili aende kuingia katika hekalu la kimwili la Mungu. Hapana, moyo wake ulitamani kitu fulani alichoona katika roho. Alisema, kwa kifupi, "Kuna uzuri, utukufu,  na msisimko juu ya Bwana sijawahi kuona katika maisha yangu. Ninataka kujua nini kinachotokeya wakati hakuna kukatishwa ushirika na Mungu wangu. Nataka maisha yangu kuwa sala ya hai."

Daudi alipomwuliza Bwana na kumwomba, "Nipate huruma juu yangu, nijibu mimi" (Zaburi 27:7), Mungu akajibu kwa maneno haya rahisi, "Tafuta uso wangu" (27:8). Hiyo ndiyo ufunguo! Unapotafuta uso wa Mungu, atakuleta katika ushirika unaoendelea, usiokatishwa pamoja na Kristo wa utukufu.