GIZA HALIWEZI KURUDIA BILA MAPAMBANO

Carter Conlon

Wakati wowote Mungu atakapofanya kitu kikubwa, watu wake watakuwa na upinzani kinyume chake. Mtume Petro alisema hivi: "Wapendwa, msifikiri kuwa ni ajabu uyo msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwambwa ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe " (1 Petro 4:12-13).

Petro alikuwa akiwaambia watu wa wakati huo, "Msifikiri ni ajabu wakati tunapaswa kupigana upinzani kama tunalenga kurudisha mambo ya Mungu katika taifa letu." Vivyo hivyo, kama wewe na mimi tunasali kwa ajili ya kuamka katika miji yetu na katika nchi yetu, tunapaswa kujiaandaa kwa kujuwa kwamba giza haliwezi kurudia bila kupigana.

Kitabu cha Kutoka kinatuambia wakati ambapo Waisraeli walikaribia kuokolewa kutoka mikono ya Wamisri. Mfalme mpya ambaye hakumjua Yosefu alikuja katika nguvu na akawanyanyasa sana. Aliwaambia watu, "Tutakuambia yale utakayoweza kujenga, na lazima uijenge kulingana na maelekezo yetu. Unaweza kwenda nyumbani yako ya ibada, lakini lazima uabudu njia yetu. Utapiga magoti yako kwa mapenzi yetu, na ikiwa unakataa, itakugharimu!" (Angalia Kutoka 1:8-11)

Hii ni sawa na upinzani ambao wewe na mimi tunakabiliwa kwa sasa, na utaona kwa kiwango kikubwa katika siku zijazo. Uhuru ambao tunajua sasa una hatari; sheria zitaanza kubadilika kwa hali mbaya zaidi. Vitisho vina uwezo wa kuzuia Kanisa la Yesu Kristo kutokana na kutambua nguvu aliyo nayo.

Hebu tumwamini Mungu kutujaza upya Roho Wake Mtakatifu ili tusiinamiye vitisho vyovyote vya uovu. Kama Bwana anatuwezesha kusimama na kuzungumza Neno Lake kwa ujasiri, tutaona kwamba ushuhuda wetu hautakuwa wetu wenyewe bali wa Mungu na Nguvu Yake ya ajabu ndani yetu!

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji aliyeanzisha Kanisa hilo, David Wilkerson, na akachaguliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.