HAKUWA UHABA KWA BWANA

David Wilkerson (1931-2011)

Mwamini yeyote anayetaka kumpendeza Mungu kwa maisha yake ya maombi lazima kwanza atatuwe swali hili: "Je, Mungu ana mahitaji yangu yote au ninahitaji kwenda mahali pengine kwa jibu langu?"

Hii inaonekana kuwa swali rahisi - labda moja ambayo halihitaji kuulizwa. Wakristo wengi wangejibu, "Ndio, bila shaka naamini Mungu anakila kitu nahitaji." Lakini kwa kweli wengi wetu hawana uhakika! Tunasema sisi tunaamini lakini mgogoro ukipiga na Mungu haonekani kuamba hayuko tayali kujibu. Mara nyingi katika nyakati hizo hatuamini kweli kwamba ana kile tunachohitaji.

Paulo anatuhimiza, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake,katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu" (Wafilipi 4:19). Bwana ana ghala la wingi ambalo linaweza kukidhi mahitaji yetu yote. Na watumishi wenye imani wanajua hili.

Mungu alitumia miaka arobaini akijaribu kuwashawishi Waisraeli kama hawatakosa chochote. Aliahidi kwamba angekuwa chanzo na ugavi wao. "Kwa kuwa BWANA, Mungu wako amekubarikia katika kazi yote mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu" (Kumbukumbu la Torati 2:7).

Mungu alikuwa anasema, "Hakuna ukosefu, kwangu hakuna uhaba. Nina kila unacohitaji, na nimekupa wewe."

"Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yuakuingiza ... nchi ... hutapungukiwa nakitu ndani yake ... Nawe utakula [ushibe]" (Kumbukumbu la Torati 8:7, 9-10).

Leo, Bwana ametuleta katika Nchi yetu ya Ahadi: Kristo! Yesu kwetu ni mahali pa kuishi ambapo hakuna ukosefu wowote. Yeye anawakilisha utimilifu wa Mungu wa kujali kimwili.

Katika Agano la Kale, waamini walikuwa na utukufu (Shekinah) wa Mungu. Lakini Mungu anasema ametoa kitu bora zaidi kwetu na kwamba ni uwepo wa Yesu mwenyewe. Yeye yuko daima ndani yetu.