HAMU YA KRISTO KWA KUWA NA USHIRIKA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alipokuwa akienda kuelekea Galilaya, alifika kwenye Kisima cha ya Yakobo huko Samaria ambako alisimama kupumzika kutoka safari yake. Wakati wanafunzi wake walipokwenda kununua chakula, mwanamke Msamaria alikuja kisimani kuteka maji na Yesu aliomba ombi lake: "Nipe ninywe" (Yohana 4:7).

Maneno ya Kristo kwa mwanamke huyu alianza kwa mazungumzo malefu na wakati wa majadiliano yao, alishangaa kwa mambo aliyomwambia. Hatimaye, akasema, "'Najua ya kuwa yuaja Masihi' (aitwaye  Kristo). "Naye atakapokuja, atatufunulia mambo yote." Yesu akamwambia, "Mimi ninayesema nawe Ndiye" (Yohana 4:25-26).

Wanafunzi waliporudi walishangaa sana kuona Mwalimu akiwa katika majadiliano na Msamaria huyo. Walianza kuandaa chakula na wakati chakula kilikuwa tayari, mwanamke huyo haraka kurudi hadi mjini. Wakamwambia Yesu, "Rabi, ule" (4:31), na Yesu akajibu kwa maneno haya ya kushangaza: "Mimi nanacho chakula msichojua ninyi" (4:32).

Yesu alikuwa akiwaambia kwamba alikuwa amelishwa chakula si cha ulimwengu huu, na alikuwa amejazwa kabisa. Alielezea, "Chakula changu ndicho hiki, niyatente mapenzi yake ya Yule alienituma, na nikaimalize kazi yake" (4:34). Vivyo hivyo, tunapaswa kuwa juu ya kazi ya ufalme wa Mungu wa kushuhudia, kutoa ushahidi na kuleta roho kwa Bwana. Yesu alikamilisha kazi hii na mwanamke Msamaria, kama Biblia inavyosema aliamini kuwa ndiye Masihi. Aliwaambia marafiki zake, "Njoni, mtazame Mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Huyu ndiye Kristo?" (4:29).

Mahitaji ya Kristo ya ushirika alikuwa anatimizwa wakati alipozungumza na mwanamke huyu. Yesu akasema, "Yote niliyoomba ni maji ya kunywa lakini aliniletea moyo mwaminifu, na wenye kutafuta. Aina hii ya ushirika ni chakula kwangu."

Yesu anataka kuwa na wakati bora na wewe kila siku. Kila wakati unamngojea, anatoa ahadi ya kuzungumza na wewe, basi subiri katika uwepo wake mpaka uisikie sauti yake inayofunua moyo wake kwako.