JE! TUNAWEZA KUWA NA KRISTO MBALI NA MWILI WAKE?

David Wilkerson (1931-2011)

Mtume Paulo anatufundisha, "Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake" (1 Wakorintho 12:27). Katika sehemu nyingine anasema zaidi hasa, "Maana kama vile mwili ni mmoja, nao unaviungo vingi ... ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo" (12:12).

Paulo anatuambia, kwa kweli, "Angalia mwili wako mwenyewe. Una mikono, miguu, macho, masikio. Wewe sio ubongo pekee, usiowekwa kwa viungo vingine. "Ni sawa na Kristo. Yeye sio tu kichwa; ana mwili na tunajumuisha viuongo vyake. Tumeunganishwa na Yesu, kichwa chetu, lakini pia tunajiunga na kila mmoja.

Paulo anatoa hoja hii nyumbani, akisema, "Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa maana sisi, ingawa wengi, ni mkate mmoja na mwili mmoja; kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja" (1 Wakorintho 10:16-17). Kuweka tu, sisi wote tunalishwa na chakula sawa: Kristo, manna kutoka mbinguni. "Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima" (Yohana 6:33).

Wakristo wengine hawataki kushikamana na viungo vyengine vya mwili. Wanazungumza na Yesu lakini wanajitenga kwa makusudi kutoka kwa waumini wengine. Lakini mwili hauwezi kuwa na kiungo kimoja tu, na mwili wa Kristo hauwezi kuwa na kichwa pekee. Hatuwezi kuwa mmoja na Kristo bila kuwa mmoja na mwili wake.

Waumini huunganishwa sio tu kwa mahitaji yao kwa Yesu, bali kwa mahitaji yao kwa kila mmoja. Paulo anasema, "Na jicho haliwezi kuwambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na nyinyi"(1 Wakorintho 12:21).

Kichwa chetu kinasema sisi ni muhimuna, hata kuwa vyenye mahitaji, kwa utendaji wa mwili wake. Hii ni kweli hasa kwa viungo ambavyo vinaweza kuharibiwa na kuumizwa. Bwana mwenyewe anasema, "Ninahitaji ninyi. Nyinyi ni viungo muhimu va mwili wangu, na kuwa muhimu kabisa kwa utendaji wa mwili huu."