JE, UNAHITAJI NGUVU?
"Je! Kufunga ninayochagua; siyo yamna hii? kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza Kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira" (Isaya 58:6). Mungu anasema kuwa kufunga anayechagua, huanza ndani ya mioyo yetu wenyewe. Tunapaswa kuwa namsimamo wenyewe wa kupokea kitu kisicho cha kawaida kutoka kwa Mungu - uhuru kutoka kwenye ukandamizaji na utumwa wa kila aina.
Waumini wanapoingia wakati wa kufunga, wanapaswa kuandaa vizuri mioyo yao ili wapokee msaada usiowakawaida kutoka kwa Mungu. Mojawapo ya sifa muhimu zaidi za kiroho ni unyenyekevu: "Kwa kuwa asema yule aliye juu na aliyeinuliwa juu, ambaye anaishi milele, jina lake ni Mtakatifu: 'Asema hivi; Nakaa mimi mahali pa juu na patakatifu, tena pamoja nayeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za watu wa nyenyekevu, na kuifufua moyo ya waliotubu" (Isaya 57:15).
"Roho iliyotubu na kunyenyekea" - huu ni moyo wa mtu anayemtafuta Mungu, ambaye anashikilia vitu vya dunia, na anajaribu kumjua Baba wa mbinguni kwa njia ya kina. Mioyo yetu imefufuliwa tunapoendelea kuwa wanyenyekevu mbele ya Bwana. Anatupatia nguvu na uzima, nguvu ya kiroho, kufurahi, upya, nguvu katika roho. "Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu na mabawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watatembea kwa miguu wala hawatafadhaika" (Isaya 40:31).
Je! Unahitaji nguvu? Je! Unahitaji Mungu atembeye kwa nguvu katika maisha yako kama hajawahi kutembea apo mbeleni? Ikiwa unakuja kwa Mungu kwa roho ya hasira, kwa kumuomba vitu kutoka kwake, hawezi kusikia sauti yako. "Mbona tumefunga, na hamuoni? Kwa nini tumejinyenyekeza, na hamujui?" (Isaya 58:3). Lakini ukimjia kwake kwa moyo uliovunjika na roho ya unyenyekevu wa kweli, anakuambia, "Naona kwamba umevunjika moyo na mimi niko hapa ili nifufuwe roho yako."