JE, UNAPATIKANA KWA MATUMIZI YA MUNGU?

Nicky Cruz

Je! Wangapi wetu tunaelewa kweli maana ya kutembea katika Roho wa Mungu, kuishi na mateso ya Yesu, kumtegemea Mungu kwa imani ambayo ni ghafi na ya kweli na yenye nguvu? Imani ambayo haijui mipaka na hofu hakuna? Imani ambayo inaweza kumtazama kwa wima shetani machoni na kusema, "Huwezi kwenda mbari! Huna udhibiti zaidi juu yangu! Wewe ni dhaifu na wazi na hauwezi! "Imani ambayo inaweza kusongeza mlima wowote, bila kujali jinsi ya urefu, upana au ugumu wake. Hata hivyo ni aina ya imani ambayo Mungu anadai kwa wale wanaotaka kuona nguvu zake. Ni jambo pekee ambalo linaweza kuamsha uwezo wa kweli na mamlaka ya Roho Mtakatifu katika maisha.

Ikiwa unataka kubadilisha ulimwengu, anza kwa kumuruhusu Mungu akugeuze wewe. Kwa kuruhusu mateso ya Yesu kuwa shauku yako. Kwa kuruhusu Roho Mtakatifu awe mwongozo wako pekee na mshauri kila hatua, kila dakika ya siku. Kwa kumruhusu Mungu kuweka moyo yako juu ya moto kwa ajili yake.

Kama waamini, tumepewa zawadi kubwa kuliko tulivyoweza kufikiria au kuomba. Tumeaminiwa kwa uwezo mkubwa zaidi kadili tunayoweza kupokea - zawadi ya Roho Mtakatifu. Roho wa Mungu! Anaishi ndani yetu, akituelekeza, akituongoza, akituwezesha kwa mambo makubwa na yenye nguvu. Na kutujaza kwa imani.

Mojawapo ya mambo makuu juu ya kumfuata Yesu ni kwamba hauhitaji kuwa tajiri au maarufu au msemaji mkubwa au mhubiri ili utembeye kwa imani na kuathiri ulimwengu. Unapaswa tu kuwa tayari kuruhusu Mungu akutumie. Unahitaji tu kuwa unapatikana wakati Mungu anahitaji mtumishi wa kufundisha au kugusa au kumsaidia mtu mwingine kwa ajiri ya jina lake. Unahitajika tu kuwa hapo. Na ni jambo lenye kuhimiza kujua kwamba yeyote kati yetu anaweza kufanya hivyo.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana, na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco: Kimbiya, Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).