Jeshi La Mungu Lililofichwa Nyakati Hizi Za Mwisho
Kuna jambo la ajabu duniani leo! Mungu yukazini anatenda jambo kwa Ukimya mafichoni – jambo lakimiujiza, binadamu hawawezi kulitafakari. Walakini, jambo hilo litatikisa dunia nzima nyakati hizi za Mwisho. Mungu anatayarisha Jeshi dogo la nguvu kati ya Wakristo! Jeshi hili ndilo litakuwa makini mno dunia nzima na Mungu atakuja kuwaongoza kutenda maajabu na kutingisa kuzimu. Mungu atamaliza nyakati akiwa na Jeshi Mabakio walio Makini na wasio na Uoga.
Maisha yangu yote nimesikia hadithi za baba zetu wa jadi waliochukia dhambi. Hawa wanaume na wanawake walitwaa masaa na hata masiku wakifunga na kuomba. Walijua vyema sauti ya Mungu. Waliomba bila kusita na walikuwa na nguvu na uwezo wa kutengana na Usherati katika siku zao. Hawa wajadi sasa hawako tena. Lakini Mungu yuko katika harakati za kuinuwa Jeshi lingine – walakini jeshi hili jipya halitakuwa la wazee wenye nyele nyeupe kutoka Zayuni. Litakuwa la waumini vijana na wazee – wakristo wa kawaida waliomkwamilia Mungu! Ni huduma mpya mno iko karibu kuja!
Kanisa la Madhehebu liko karibu kufifia. Halina uwezo wowote wa kuigeuza Dunia, Halina nguvu za Krito. Makuhani wengi wanaanguka kila wakati – kwa Usherati, tamaa, kiburi na ngono za aina yote. Wachungaji wa kiinjilisti wameleta maburudisho na maonyesho katika madhabahu. Mchungaji mmoja akaringa, “Ninataka kuwaletea watu wa michezo ya Broadway hapa Kanisani”. Mimi najua makanisa ya Kiinjilisti ambapo takriban asilimia 50 ya waumini wao wamekwisha vunja ndoa. Mahali kwingine, inafika hata asilimia 80 kulingana na Barua za waumini ninazopata. Washerati, wapenda ngono na wachawi – yote haya yameinyemelea kanisa la Yesu. Wengine wananilaumu kwamba niko mkali sana kwa wachungaji. La sivyo – kwa sababu niko na wachungaji wengi wale wanao lia kama mimi kuhusu kuanguka kwa huduma enzi hizi zetu. Kuna Mabakio ya Wachungaji nchini mwetu. Nashukuru kwa kila moja wao. Ni wazi kwamba wachungaji wengi wanaelekea katika njia hii ya ulegevu na ufisadi na hata sasa Dunia inaicheka Nyumba ya Mungu. Shetani anaringa kwamba ameshinda vita kwa sababu ya utoaji mimba kisheria, ushoga, ulevi, kuabudu shetani na uisilamu.
Walakini Bibilia inasema tusiogope! Mungu yuko na mpango, na Mpango wake umeanza kuenea. Mpango huu uko katika Neno. Kwa kweli, kila pepo kuzimu anajuwa Mpango huu!
Mpango Huu Wa Mungu Unapatikana Katika Sura Nne Za Mwanzo Katika Samueli Wa Kwanza.
Nabii Samueli ni mfano wa Mabakio wa Mungu. Mungu alimchagua katika nyakati mbaya zaidi akamficha na kumfunza mpaka ikatimia wakati wa kufichua Jambo jipya! Mungu akamwambia Samueli, “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe”(Samueli wa Kwanza 3:11). Hili Jambo jipya lilipangwa kuwashangaza na kuwashutua wale watakao lisikia. Jambo hili lilikuwa lipi? Lilikuwa Hukumu ya Mungu kwa dini duni iliyoanguka – na kutayarishwa, kuinuliwa na kupakwa mafuta kwa Mabakio watakatifu!
Sasa tazama yale Mungu alitenda wakati wa Samueli, yeye hutenda haya katika kila kizazi. Wakati kanisa la kidini linapoanguka, kulegea na kuwa baridi, Mungu analitosa nje na kuinua lengine. Kila kizazi kimekuwa na mabakio watakatifu, wale waombezi walio karibu na Moyo wa Mungu. Eli na watoto wawili, Hofni na Finehasi, walisimamia Kanisa lililopotoka kwa njia za Mungu. Bibilia inatuelza “Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu BWANA (Samueli wa kwanza 2:12). Vijana hawa walimdharau Mungu. Walitenda Usherati katika milango ya Hekalu! Wanawake walipokuja kumtumikia Mungu, wana wa Eli waliwatega kando na kuwahadaa. Watu hawa hawakumuhofu Mungu – walikuwa wanatumikia kana kwamba ni kazi tu ya kawaida.
Lakusikitisha zaidi ya yote ni kwamba Baba yao aliangalia kando! Eli alikuwa karibu miaka 90, alikuwa amenona, yuko starehe na mgumu wa moyo. Alikuwa amezoea nyama nono aliyopata kutoka kwa waototo wake. Eli alijua nyama hii imelaaniwa – lakini hakutenda lolote kuzuia watoto wake kuiba. Alifunga macho asipate kuona Usherati wao. Hii ndiyo picha ya uovu ambayo imekumba kanisa la leo. Madhehebu yanajadili kuwapa mashoga madhabahu. – na kuleta laana katika nyumba ya Mungu. Eli na watoto wake wanasimamia, ukuhani uliokufa, wenye mitindo baridi wanaobembeleza dhambi. Wanatenda tu sasa matakwa ya huduma. Wakiwa na uungu uliyokosa nguvu. Ni kwa sababu wamekuwa starehe pale walipo! Wamepoteza Mguso wa Mungu na sasa hawasikii tena sauti yake. Kwa sababu wanafungia macho maovu. Mungu akasema, “Kwa kuwa nilimwambia (Eli) kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia.” (Samueli wa Kwanza 3:13). Kwa sababu Eli alikataa kuhukumu na kusahihisha maovu, Mungu alimng’oa kutoka kwa Mamlaka yake ya kiroho. Hili ndilo linalotendeka sasa katika kanisa ka Yesu kristo.
Wakati mchache uliopita niliongea na wachungaji wa Kipentekoste waliotembelea kanisa letu. Nilipowaeleza kuhusu ukosefu wa Kukemea dhambi, mkuu wa kundi hilo aliangusha tu kichwa chake. Mchungaji mmoja akatubu: “Ndugu Dave, ninaogope kwamba nikisema ukweli, nusu ya waumini watatoroka.” Kila mmoja ya watu hawa walikuwa wapole sana kwa waumini wao – wakiogopa kuwakwaza! Naweza kusema kwa hakika, sijaona hata wazee kumi wenye nyele nyeupe walio na motisha ya kulia kinyume na dhambi. Majeshi wengi wa Mungu ni kana kwamba wamekufa kiroho au wanaelekea kufa. – wamejipanga mbele ya Runinga, wamevuja nguvu zote kwa roho za dunia hii. Wamekuwa Eli – wakilala fofofo, wakinona na kufanikiwa, waoga wa kupinga dhambi!
Mungu Alikuwa Amechoshwa Na Kizazi Cha Eli!
Mungu alituma Nabii kumuonya Eli: “Wakati unakuja nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika mbari yenu atakayeishi kuuona uzee (Samueli wa Kwanza 2:31). Mungu alikuwa akisema, “Ninajitenga na Nyumba hii — ninatoa uwepo wangu, nitakufanya bila nguvu na kuhukumu wachungaji wako. Nitapatiana ibada zenu duni kwa adui! “nanyi mtaona huzuni katika makao yangu. …” (mstari wa 32).
Wakati huu, pesa za Muungano wa makanisa zinatumiwa kusaidia wapiganaji vita ulimwenginu mwote. Na tunashangazwa ni kwanini Kanisa la Amerika halina mamlaka ya Kiroho wala Uongozi! Madhehebu mengi yamekuwa kama makaburi na nyumba ya maiti. Hazina maisha, wala nguvu kwa sababu Mungu amewakwepa! Kanisa la Eli – Kanisa la Shilo – ni mfano kama huu. Mungu alilihukumu na kulikwepa kanisa hilo, yote yakifanyika kwa siku moja. “...Israeli wakapoteza askari 30,000 waendao kwa miguu. 11Sanduku la Mungu likatekwa, na hao wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, wakauawa. (Samueli wa Kwanza 4:10–11). Mungu alisema: “Imetosha!” na katika siku moja, Sanduku la Mungu lilitekwa nyara. Inalingana na kotoka kwa uwepo wa Bwana. Utukufu wa Bwana ulutoweka – Ikabodi akazaliwa – na Mungu akahukumu huduma duni kwa haraka! Eli alisikia habari kuhusu Sanduku kutekwa nyara, “...Mara alipotaja sanduku la Mungu, Eli alianguka kutoka kwenye kiti chake kwa nyuma kando ya lango. Shingo yake ikavunjika naye akafa, kwa kuwa alikuwa mzee tena mzito. (Samueli wa Kwanza 4:18).
Hili ni picha nzuri ya yale yanayo tendeka kati ya madhehebu Amerika. Dini iko katika hukumu – wachungaji wanaanguka kulia na kushoto, viongozi wao wamekufa kiroho. Utukufu wa Mungu umetoweka – na kanisa limejipatiana kwa adui!
Ni kama siku za Yeremia. Watu wa enzi hizo walisema, “tuko sawa – hatuko hatarini. Hatutapoteza wokovu wetu”. Lakini Mungu alinena kupitia Yeremia: “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, 10kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii, inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.’’ Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza? Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyang'anyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! Asema BWANA. “ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli. (Yeremia 7:9–12).
Katika kila kizazi Mungu huonya kanisa baridi zilizo chafu: “Rudini Shilo – rudini katika kanisa la Eli. Tazama yale niliyoyatenda kwa Hofni na Finehasi! Tafakari yaliyotendeka nilipotoa Uwepo wangu, Utukufu wangu utaondoka kila mara dhambi itakapoingia kwenye Kambi!”
Bali wakati kanisa la Eli lilipokuwa katika hukumu, Mungu alikuwa akishughulika na kuinua Mabakio takatifu! Samueli anasimamia Mabakio takatifu – mwili wa waumini unainuka kutoka kwa vifusi la kanisa zee lililokufa. Nataka kuwaonesha yale mambo muhimu katika Ukufunzi wa Mabakio watakatifu wa siku hizi za Mwisho
1. Mabakio Huzaliwa Katika Maombi Na Maombezi!
Hana alimzaa mwanawe kwa machozi na Maombi: “Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba BWANA. (Samueli wa Kwanza 1:10). Jaribu kutafakari mahala pale: Hana yuko kwa hekalu kila siku, magotini, mbele ya madhabahu, amevunjika kwa sababu hana mtoto. Anapolia, mke mwenza Penina – alimchokoza. “...Kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake alikuwa anamchokoza ili kumwudhi. Samueli wa Kwanza 1:6)
Kuna mambo matatu muhimu ningependa kusema kuhusu tukio hili:
Kwanza, Mabakio takatifu inayosimamiwa na Samueli, huzaliwa kwa Majonzi na Maombi
La pili, wale waombao na kulilia Mungu watachokozwa na maadui.
Na la tatu, Mabakio takatifu wa Mungu kila mara hukosa kueleweka! Tafakari yalimtendea Hana alipokuwa katika maombi:
“Alipokuwa anaendelea kumwomba BWANA, Eli alichunguza kinywa chake. 13Hana alikuwa akiomba moyoni mwake midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.” (Samueli wa Kwanza 1:12–14). Eli alikuwa mbali na Mungu – alikuwa amekufa kiroho – alifikiri Hana amelewa! Akamueleza, “Mama, utaendelea kwa mda gani kuja ukiwa hivi kanisani, tupa chupa ya ulevi!” Jambo hili linanishangaza mimi! Eli hakuweza kukosoa watoto wake kwa ulevi na usherati – lakini alimdhania Mwanamke wa Mungu kuwa mlevi! Hakuna tofauti na siku hizi zetu. Wakristo walio Makini wamejipatiana kwa maombi, wanatembea wakiwa kando pamoja na Yesu – lakini wachungaji ndiwo hugeuka na kuwa vizuizi, wakiwahadaa na kuwadhihaki!
Hana alipokuwa mbele ya Madhabahu, alijaa Uchungu, alililia mtoto. Lote aliloweza kufanya ni kusongeza mdomo tu kulingana na majonzi yaliyomo Rohoni. Aliomba, “...Ee BWANA Mwenye Nguvu, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa BWANA kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake. (Samueli wa Kwanza 1:11). Kama utampenda Mungu kwa Moyo, Nafsi, Akili na Nguvu zako zote, Basi kama Hana, utasikia uchungu wa Mungu na Kanisa lake. Mungu alimsikia Hana! Hii ndiyo maana ya jina Samueli: “Mungu alisikia Maombi yangu!” Siku hizi pia, Mungu anasikia maombi ya wale wanaolilia kuzaliwa kwa Kanisa takatifu, Jambo jipya la Roho Mtakatifu. Waumini hawa wanataka kuona Mungu akitenda jambo la ajabu – na Mungu atasikia kilio chao! Kutoka kwa tumbo la uzazi wa kiroho ya majeshi wasiojulikana la waombezi, mwili wa waumini unaendelea kuzaliwa – Kundi la Samueli, wale waliojipeana kabisa kwa Mungu!
Mambo mawili kuhusu Mabakio takatifu wa Mungu:
1. Wanaomba kama Hana: Mzigo wao ni wa kimo kirefu na mioyo yao imechokorwa kwa sababu ya dhambi ilioko kwa nyumba ya Mungu.
2. Na kama Hana, wamejipena kwa maombi kila siku. Si kana kwamba wako juu mara chini, moto mara baridi. Hapana – wamejipeana kamili kwa Mungu. Wanamuendea na kumwaga yote yalio moyoni mwao: Enyi watu, mtumainini Yeye, wakati wote, mmiminieni Yeye mioyo yenu…” (Zaburi 62:8). “Vitu hivi ninavikumbuka ninapoimimina nafsi yangu: …” (Zaburi 42:4).
Samueli akawa shujaa wa maombi – mpaka waisraeli hawakumuuliza mashauri bali walimuuliza awaombee! Maandiko yanasema, pale watu walipotaka Mfalme, “...Kisha Samweli akamwomba BWANA na siku ile ile BWANA akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana BWANA na Samweli. Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako, kwa ajili ya watumishi wako ili tusije tukafa,kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”(Samueli wa Kwanza 12:18–19). Kila mara tunaona watu wakimsihi Samueli, “Tuombee.” Ni kwa sababu walikuwa wameamini maombi yake! Na katika nyakati hizi za mwisho, kutakuwa na Mabakio ya waombezi ambao watatafutwa na watu kwa sababu ya maombi, watu watakimbia wakilia, “Najua mtu awezaye kumgusa Mungu!” Kushauri pekee haita tekeleza matakwa ya watu. Itakuwa ni maombi ya watu wanao jua mawazo ya Kristo.
Mkristo mpendwa, Mungu anataka kukufanya mtu huyo! Anataka uweze kumgusa na kumsikia. Anataka kukupatia Huduma kutumikia wengine walio na mizigo na majaribu. Unapowaombea, neno lake litakuja!
2. Mabakio Takatifu Wamefunzwa Kujua Sauti Ya Mungu!
Mungu alikuwa haneni na waisraeli kwa sababu ya dhambi ya wakuhani na waumini. Bibilia inasema: “Katika siku zile Neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi” (Samueli wa Kwanza 3:1). Lakini, katikati ya ukame wa Neno, Mungu alimnenea Samueli: “...BWANA akamwita Samweli ...........Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua BWANA. Neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. (Samueli wa Kwanza 3:8, 7). Samueli alikuwa miaka 12 wakati huwo, ingawa alikuwa mtoto mtiifu, hakuwa ameijua sauti ya Mungu. Basi Mungu alikuja kando ya Kitanda chake na kumwita. Samueli alifikiri ni Eli anayemuita. Hakujua alikuwa anafunzwa kutofautisha sauti – kusikia moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
Tafakari haya. Mungu alikuwa hamuongeleshi Eli! Kwa kweli, hadi sasa, ni Nabii mmoja tu alikuwa akisikia kutoka kwa Mungu – yule ambaye hakutajwa jina aliyemuonya Eli kwamba Mungu anataka kumuhukumu. Hata Nabii huyu alikuwa mtu, ni sauti ya mtu pekee Eli angeweza kusikia –kwa sababu alikuwa kiziwi kwa sauti ya Mungu! Ndivyo ilivyo leo! Huduma ya eli, imekufa kiroho na kulala, imepoteza umakini na mamalaka, nguvu zote za Mungu zimetoweka. Kanisa linahitaji leo Waume na Wake wanaoweza kusimama na Mamlaka ya kiroho – kwa sababu Neno wanalohubiri limeinuliwa katika maisha yao matakatifu! Waubiri wengi leo hawawezi kusimama mbele ya waumini na kusema, “Ndivyo asemavyo Bwana!” – kwa sababu hawako karibu na sauti ya Bwana! Kusikia kutoka kwa Mungu inachukua zaidi ya nyakati za kimya pekee. Inachukua zaidi ya kusema tu, “Ongea Bwana, kwa sababu mtumishi wako anasikia!” Hapana, hakuna mipangilio maalum ya kumsikia Bwana – hakuna mikakati ya Kufuatilia, kabla hujamsikia Bwana, inalazimu kuwa yeye Bwana anaongea nawe!
Eli labda angelichukua miezi kadhaa pekee, akilia, “Bwana, Ongea nami!” lakini hakuwa na nafasi ya kumsikia Mungu – kwa sababu Mungu alikuwa haongei naye. Mungu alikuwa anataka kuongea na Samueli. Anaongea na wale ambao wametayarisha mioyo yao kusikia! Wauburi walio chafuka akili hawata wahi kumsikia Bwana. Waumini wale wanaovunja ndoa, washerati, wanaofanya sana michezo, kujiburudisha na kujifurahisha hawatamsikia Bwana, lile atakalo wanenea ni hili, Tubuni, Rudini! Lieni!”
Samueli hakuwa msomi wa kidini Mungu alipomuongelesha. Lakini alikuwa na moyo mkunjufu, wa upendo uliokuwa wazi kwa Bwana. Unafikiri ni kitu gani Mungu alimfunza Samueli alipomuongelesha? “Sitakaa na dhambi katika nyumba yangu! Sitafunga macho kwa dhambi kati ya watumishi wangu.” Kwa ufupi, Mungu alimwambia Samueli, “Nitamuhukumu Eli – kwa sababu yeye na watoto wake ni waovu, naye Eli hakutenda jambo kuwazuia! Ingekuwa vyema wakivuliwa nguo za utumishi na kuambiwa, “hamuwezi kuenda hapo patakatifu! Samueli, sasa nataka kukuonesha chuki yangu kwa dhambi ndani ya nyumba yangu. Nataka nikuoneshe ni vipi utawahi kusikia sauti yangu na kutembea nami!” Samueli lazima alishutuliwa na mambo Mungu alitamka baadaye: “Naye BWANA akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe.” (Samueli wa Kwanza 3:11). Samueli aligundua kuwa Mungu atamkana Eli, mtu ambaye samueli alikuwa ametazamia. Moyo wa kijana huyu lazima uliguswa kwa majonzi pale Mungu alipomnenea, “Nitawaharibu watumishi waovu, nakuinua watu wanaonitafuta!”
Mabakio takatifu nyakati hizi za mwisho wanajua kwamba Mungu anahukumu kanisa. Na wanaijua mpango wa Mungu. Wanajua kwamba Mungu atazivunja na kubomoa huduma mbovu za watu waovu! Si ajabu Bibilia inasema Samueli aliongea mambo ya Ukweli – alikuwa amesikia kutoka kwa Mungu! Alikuwa amechukua mda akiomba, akimtafuta Bwana, akajifungia naye – na Mungu akamuongelesha kila wakati. Kuna watu watakatifu wakati huu ambao wamefunzika kuijua sauti ya Mungu. Waombezi hawa wanamwaga mioyo yao kwake – naye Bwana anaimwaga Roho yake kwao!
3. Mabakio Takatifu Watafunzwa Ukombozi Wa Kweli – Kupitia Ujuzi Wa Njia Za Bwana!
Nimeonya mara nyingi, Amerika inaelekea Janga na Kuporomoka! Waubiri wa chuki kama Louis Farrakhan wamejulikana sana sasa kati ya waamerika wausi kulingana hata na Jesse Jackson. (Farrakhan sasa anjulikana kushinda Martin Luther King!). Radio nyingi za waamerika wazungu hata hapa New York zinaubiri chuki kwa waafrika. Labda umesoma au kusikia maubiri yangu kuhusu vita vya kikabila. Kwa sasa inakaa kana kwamba hili haliwez kutokea. Lakini pale uchumi utakapo fifia, kaa chonjo! Kutakuwa na “majeshi ya kikabila” – wazungu wakipinga waafrika, wafrika wakipinga wayahudi, wakorea wakipinga waafrika. Tunapitia wakati wa hukumu hadi neno Ukombozi litapata maana tofauti kabisa! Wakati uliopita, wakristo wamechukulia Ukombozi kama uponyaji wa kimwili – macho yakirejeshwa, miguu ikiponywa. Hapa karibuni kutatokea hukumu kutoka mbinguni mpaka Ukombozi mkuu utakuwa kutokana na Uoga na Vitisho! Ukombozi wakati huwo utakuwa ni kuwa na neno kamili kutoka Mbinguni. “Yesu alisema mioyo ya watu itawapotoka kwa uoga wa yale mambo ya kutisha itakayoikumba ulimwengu. Na kweli, watu watashindana kujua mpango wa Mungu, watakimbilia njia zote wakitaka kumsikia yule aliye tulia, aliye na Amani, asiye kuwa wazima, na watalia, “Niambiye, je ni Mungu anahukumu? Yataisha lini haya yote?
Na unafikiri nani atakuwa na jibu? Wewe – Mkristo wa kawaida ambaye amejificha ndani ya Bwana! Utakuwa mtulivu na mwenye amani wakati mambo yanaporomoka – kwa sababu Mungu yu nawe, unasikia kutoka mbinguni. Aliwaonya nyote kwamba haya yatatendeka – na aka ahidi kuwatetea! Niko na maono mawazoni mwangu ambayo naamini yametoka kwa Bwana Mungu. Ni ya magari mengi yakitoroka New York...ya kambi ya magari New Jersey na Pennsylvania...ya watu wakilala kwa magari yao kwa mawiki, kutoroka misukosuko hii. Haya yatatendeka kwa miji mingine pia. Itakuwa Janga kupita yale tumekwisha wahi kuona. Lakini Mungu atawaweka tayari Mabakio takatifu – watu walio makinika, wakweli, walioimara kabisa! Kama Samueli, maneno yao hayatapotea ardhini!
Samueli alikuwa na majibu kwa waisraeli; aliwakabidhi Ukombozi wa kweli. Zaidi ya watu 50,000 walikwisha kufa kwa sababu ya kuchungulia katika Sanduku la Bwana. Pale sanduku lilipoenda watu walikufa kama nzi – hakuna aliyejua la kufanya. Watu wakasema, “Hukumu hii lazima iwe kutoka kwa Mungu! Nani ataenda mbele zake kwa niaba yetu?” kwa hivyo wakamtumania Samueli naye, akawaambiya, “nataka mkusanyike Mizpah. Hapo nitawaonyesha njia ya kutokea” Samueli alikuwa na maneno ya sawa kulingana na Janga lililo kuwepo. “Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa BWANA na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.’’ Hivyo Waisraeli wakaweka mbali Mabaali yao na Maashtorethi nao wakamtumikia BWANA peke yake.” (Samueli wa Kwanza 7:3–4).
Jibu halitapatikana kwa kuombea kila mtu, hata wakiwa dhambini kiasi gani. Hapakuwepo na Ukombozi kwa yeyote aliyetaka. Hapana – Samueli alilia, “Elekeza moyo wako sawa, na hukumu dhambi yako! Tayarisha moyo wako kwa Bwana! Kwanza dhambi lazima ikanywe, ihukumiwe na iachwe. “Kisha Samweli akasema, “Wakusanyeni Israeli wote huko Mispa nami nitawaombea ninyi kwa BWANA.’’ (Samueli wa Kwanza 7: 5). Watu wakafunga na kunyenyekea mbele za Bwana: “Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na wakaungama wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya BWANA.’’ Naye Samweli alikuwa kiongozi wa Israeli huko Mispa. (Samueli wa Kwanza 7: 6). Aliwahukumu – Samueli alifichua dhambi yao kambini! Ufifio wa ukweli ulifuata Kemeo la Samueli.
Mungu anatueleza, Kambi ka Samueli litaleta Ukombozo wa ajabu kwa nguvu za maombezi: “…Kisha Samweli akamchukua mwana kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kama sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Akamlilia BWANA kwa niaba ya Israeli, naye BWANA akamjibu. Wakati Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile BWANA alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli.” (Samueli wa Kwanza 7:9–10). Hii ilikuwa ngurumo kutoka mbinguni, ikifwatwa na Ushindi mkuu – watu wa Mungu walipata Ushindi! Ilitendeka tu kwa sababu mtu mmoja alijua jibu. Samueli alijua la kufanya – kwa sababu alisikia kutoka kwa Mungu!
Naamini Mungu atatumia Mabakio takatifu wake kutingisa umati wa watu, kuamsha wachungaji na makanisa. Majeshi haya yatarudisha mioyo ya wengi kwa Mungu kwa kuwaleta katika Toba – kupitia nguvu maombi na Kukemea kwa dhambi. Jirani zako na wafanyikazi wenzako wote watataka majibu. Wanakujua tayari kwa sababu ya Amani na Utilivu wako – siku moja watakuja mbio kwako, wakilia, “Neno gani kutoka kwa Mungu? Mungu anasema nini? Nikinena kuhusu Mabakio walio mafundishoni, si maansihi jeshi la waubiri neno, wainjilisti, au wamishonari. Ninamaanisha Mkristo wa kawaida – wanao mpenda Yesu, ambao wao wenyewe watakuwa vielelezo vya kimiujiza ulimwenguni, waliojaa Amani na Utulivu. Mungu hataki wasomi waliofunzwa na njia za kidunia. Anataka Waume na Wake waliofunzwa katika maombi na Roho Mtakatifu! Anatafuta wale waumini walio jificha pamoja naye, wakitayarisha mioyo yao mbele zake, wakisomea kusikia sauti yake.
Je, mambo haya yanalingana nawe? Maisha yako hivi sasa ni Ushuhuda Duniani palipo na kutikiswa na kuogopa kwingi? Nakusihi – nenda kando pamoja na Mungu ili akuongeleshe, muulize akueleze dhambi iliyo katika maisha yako. Acha kabisa yote yale Roho Mtakatifu atakusihi moyoni. Jitoe kwake na uanze maombi. Kisha utakuwa tayari kama Jeshi, katika Jeshi lake kuu la siku hizi za mwisho. Hallelujah!
---
Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation - http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)