KAZI YA KWANZA YA ROHO MTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Isaya anatabiri kinachotokea wakati Roho Mtakatifu anashukia watu. "Roho humwagwa juu yetu kutoka  juu, na jangwa kugeuka shamba lenye kuzaa, na shamba lenye kuzaa linahesabiwa kama msitu" (Isaya 32:15). Anasema, "Wakati Roho Mtakatifu atakapokuja, hapo zamani jangwa liliokuwa tasa litageuka shamba la mavuno. Kipande kilichokufa cha ardhi ghafla kinatowa matunda, na shamba hilo la matunda litakua ndani ya msitu; utakuwa na uwezo wa kuchukua vipandikizi kutoka mwaka huu wa misitu baada ya mwaka na kujenga juu ya matunda yako daima."

Wakati Roho Mtakatifu anapokuja, kazi yake ya kwanza ni kusafisha kanisa lake. Hiyo ndiyo yaliyotokea wakati wa Pentekoste. Petro alipoanza kuhubiri kwa upako wa Roho, watu walihukumiwa sana na wakalia, "Tufanye nini?" (Matendo 2:37). Jibu la Petro lilikuwa, "Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo kwa msamaha wa dhambi zenu" (Matendo 2:38). Maelfu walikuja kwa Kristo siku hiyo kwa sababu walitambua dhambi zao na walitaka uhuru.

Wakati Roho Mtakatifu anaanza kushughulika na mambo katika kanisa la Yesu Kristo, anafanya hilo kwa upendo kwa kila mtu, akiwahukumu kwa kila sanamu, kila hatua ya nafsi inayojikuza yenyewe kwa kupinga ufahamu wa Mungu.

Isaya anaendelea, "Basi ndipo hukumu jangwani, na haki itabaki katika shamba lizaalo saana" (Isaya 32:16). Isaya hazungumzii kwa wakati mmoja juu ya kumwagiwa kwa Roho, kile ambacho watu wanaweza kufikiria kama "uamsho." Hapana, anaelezea kitu kinacholeta mabadiliko ya kudumu.

"Kazi ya haki itakuwa amani, na matokeo ya haki, utulivu na matumaini ya milele. Na watu wangu watakaa katika makao ya amani, katika makaazi yenye kuwa salama, na katika mahali pa kupumzika penye utulivu" (32:17-18). Roho Mtakatifu ndiye msimamizi wa amani ya Kristo - hutoa amani - na hapawezekani kuwa amani bila haki.

Ninakuhimiza leo kuomba zaidi Roho Mtakatifu katika maisha yako. Omba ili abadirishe nafsi yako na kukuelekeza kwenye chumba chako cha siri. Yeye atakupatia mapumziko yenye utulivu na uhakikisho amabao atakuona kupitia chochote kitakuja.