KAZI YA MUNGU KATIKA MAJARIBU YETU YOTE

Gary Wilkerson

"Mnafurahi sana wakati huo, Ijapo kuwa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali; ili kwamba jujaribiwa kwa Imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hio hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Naye mwampenda, ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoonekana, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa Imani yenu, yaani wokovu wa roho zenu" (1 Petro 1:6-9).

Petro anasema kwamba ni muhimu kwetu kupitia jaribio kwa muda mfupi. Natamani kwamba ni ngefanya matatizo yote kuwa katika maisha yangu kwa muda, Je! Wewe? lakini Petro hazungumzia juu ya muda mfupi, anasema kwamba wakati sisi tuko hapa duniani, hatuwezi kukimbia majaribio ya moto ambayo hutufanya kuwa wasiwasi na kuwa na misukosuko. Wakati sisi bado tuko katika mwili huu tusifikiri kwamba nikitu kisichokuwa cha kawaida kwa kuteseka. Mungu anajua na kwa kweli atafanya kitu cha nguvu katikati majaribu yetu.

"Katika hili furaheni" (mstari wa 6). Kwa nini mtu anapaswa kufurahi akiwa ndani ya majaribu na mateso? Katika Kigiriki neno furaheni kama lilivyotumika hapa linamanisha kurukaruka kwa furaha. Neno hilohilo linatumiwa katika kitabu cha Matendo wakati mulemavu aliponywa na petro kwa mtia mikonojuu yake (tazama Matendo 3:9). Lengo ni kukidhi changamoto ya kuwa na uwezo wa kukubaliana na wewe. Wanaume watatu wa kiebrania walitupwa katika tanuru ya moto lakini badala ya kuteketezwa na moto, walikuwa katika hali kamili - kwa utukufu wa Mungu. Hata mfalme alivutiwa na imani yao imara katika Mungu wao (angalia Danieli 3:20-29).

Tunapenda kusoma ushuhuda huu, lakini Mungu ni ule ule leo kama alivyokuwa wakati huo. Anakwenda nasi kupitia majaribio yote na anatuleta kupitia ushundi kama tunamuamini kabisa.