KILIO KUTOKA NDANI YA ROHO YAKO YENYE HUZUNI

David Wilkerson (1931-2011)

Je, Unaamini kama Mungu yuko tayari kurudi haraka kutatua tatizo lako? Hapa ndio Wakristo wengi wanapungukiwa. Wanajua Mungu anamahitaji yote wanataka, na wanakubali kuwa anajali. Lakini wakati hajibu kilio chao kwa njia sahihi, wanafikiri juu ya aina zote za sababu kwa nini hataki kuwa tayari kuja kuwasaidia.

Kwenye Mlima Karmeli, Eliya alinena kwa ujasiri juu ya Mungu wake. Aliwadharau manabii wa Baali kwa kumshtaki mungu wao ka mtoto asiejali: "Wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, ' Ee Baali, utusikie!' Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. ... Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyiya zihaka, akusema,” Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo, labda anazungumuza, au ana sughuli, anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe.

"Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao ... hata damu ikawachuruzika ..."Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala iliyeangalia" (1 Wafalme 18: 26- 29).

Sikiliza maneno haya tena: "Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala iliyeangalia."

Cenye Eliya anaonesha, nijinsi tunashtaki Mungu. Tunasali, tunamlilia Mungu kwa sauti, lakini tunakwenda njia yetu, nakutokuamini kwamba amesikia. Tunakwenda mbali na uwepo wa Bwana - mbali ya kujifungania mahari pasiri kwa maombi - kushangaa ikiwa amejali kwa makini malalamiko yetu.

Bwana yuko tayari siku zote kwkusikia na kujibu kilio chetu cha kutafuta msaada. Ninampenda kile Daudi alichosema juu yake: "Kwa maana Wewe, Bwana, umwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa wote wakuitao ... Siku ya mateso yangu nitakuita, kwa maana utaniitikia."(Zaburi 86:5, 7).

Mungu anasubiri kilio chako kutoka moyo wenye huzuni nyingi, umekamilika kama imani ya watoto.