KRISTO ANAENDELEA KUWA MFALME

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu Baba alimutawaza Kristo kuwa mfalme wa mataifa yote na asili yote, na kama Bwana juu ya Kanisa. Mtume Paulo anaandika kwamba wakati Yesu atakapokuja tena, "Ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uwezo peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa ma Bwana" (1 Timotheo 6:15).

Paulo anasema kwamba haijalishi mambo yanavyoonekana kwa nje, ukweli ni kwamba, Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu ya Yesu na bado ni mfalme juu ya kila kitu. Kila kitu kinaonekana bila ya kudhibiti na inaweza kuonekana kama shetani amechukua nguvu, lakini si kweli. Hata hivyo, karibu na sisi leo, tunaona jumuiya yetu na serikali imemuondoa Kristo kwenye kiti cha enzi - kukataa kukubali mamlaka yake na utawala wake. Tumeondoa Mungu kutoka shule zetu na mahakama na kumchukia katika kuunda sheria zetu. Na sasa tunapata mavuno mabaya sana.

Kwa kusikitisha, wasiwasi wangu huenda zaidi ya kukataa kwa mamlaka ya Yesu. Ninaona shida ndani ya Kanisa kuwa mbaya zaidi. Inaeleweka kwamba watu wasiomcha Mungu hutaka kuondowa Kristo kwenye kiti cha enzi; Inafahamika kwamba watu wasio mcha Mungu wanataka kuondoa Kristo kwenye kiti cha Enzi; waritukana na kulizalau jina lake tangu siku aliyozaliwa. Lakini huwumiza Mungu kuona Kristo akiwa akiondelewa kwenye kiti cha enzi na wale wanaojiita kwa jina lake.

Polepole lakini kwa hakika Wakristo wengi, makanisa na huduma wanakataa shauri la Bwana. Hawategemee tena utawala wake kabisa. Badala yake, wao wanageukia hekima ya ulimwengu, kwa mambo anayobuniwa na watu. Nimeangalia kwa makini Kanisa likiweka polepole hekima ya ulimwengu. Yesu sio tena chanzo na nguvu nyuma ya watu wa Mungu.

Hebu acha nikuulize wewe mwenyewe binafsi: Je! Umemuondoa Kristo kama mfalme wa moyo wako? Ninakuhimiza leo kumweka Kristo kwenye kiti cha enzi cha moyo wako - na kuishi! "Nitayainua macho yangu nitazame milima - Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliezifanya mbingu na nchi " (Zaburi 121:1-2).