KUACHIA MAJUTO KATIKA NYAKATI ZA NYUMA
Maandishi ya mtume Paulo yanaonyesha wazi kwamba hamu yake kuu katika maisha yake ilikuwa ni kumjua Yesu. Alitaka kujitolea kikamilifu kwa Kristo aliye hai ambaye alikuwa akijua kuwa alikuwa amekaa ndani ya mwili wake wa kidunia. Aliandika, "Kwa maana ndani yake tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu" (Matendo 17:28).
Paulo alikuwa anajua kitu tunachohitaji kugundua upya leo: Hatujaitwa kuleta tu maarifa ya Mungu kwa kizazi chetu; Tumeitwa kuwa dhihirisho dhahiri la Mungu ni nani, kwa kumruhusu aonyeshe nguvu, hekima, neema na upendo kupitia sisi.
Paulo pia alitamka jambo ambalo linapaswa kutia moyo wakati wowote tunapohisi ujinga unaolinganishwa na yale tunayosoma juu ya Bibilia: "Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha mkamilifu" (Wafilipi 3:12). Kwa kweli alikuwa akisema, "Mimi sio kila kitu ambacho ningelipaswa kuwa." Paulo hakukuwa hivo - na sisi hatuko hivo! Lakini aliendelea na jambo lenye kutia moyo sana: "Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile amabalo kwa ajili yake nishike yale ambayo Kristo Yesu amenishikilia pia kwa ajili yangu ... nikiyasahau mambo yaliyo nyuma, na kuyafikia mambo ambayo yako mbele, nakaza mwendo, nifikiye mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (3:12-14).
Kwa maneno mengine, "Mungu ana mpango wa maisha yangu, na ninasonga mbele kutimiza yale ambayo Kristo ameamua kufanya kupitia kwangu." Mojawapo ya mambo magumu kwetu ya kuacha nyuma ni kujuta kwetu. Sisi huachunga kwa kuyabeba kupitia maisha - mawazo hayo ya mara kwa mara ya, "Laiti ningekuwa nimefanya hivi; laiti ningekuwa hivi; kama tu sikuwa na ubinafsi.” Na orodha inaendelea na kuendelea.
Paulo alikuwa na sababu nyingi za kuishi katika majuto. Kwa mfano, anasema, "Maana mimi ni mdogo kabisa katika mitume, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nilitesa kanisa la Mungu" (1 Wakorintho 15: 9). Na katika Matendo 26:10-11 anaorodhesha hata zaidi makosa yake. Lakini alifanya uamuzi wa makusudi kusahau vitu ambavyo vilikuwa nyuma yake na kwenda mbele na Yesu! Vivyo hivyo, unaweza kuchagua kuweka makosa yako yote ya zamani msalabani na kutembea mbali na majuto yako. Alikufa ili akupe akili mpya na moyo mpya - ipokee kwa imani!
Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa Kanisa la Times Square mnamo 1994 katika mwaliko wa mchungaji mwanzilishi, David Wilkerson, na aliteuliwa kuwa Mchungaji Mwandamizi mnamo 2001.