KUCHIMBA ZAIDI NDANI YA UPENDO WA MUNGU KWA AJILI YAKO
"Bali nyinyi wapendwa, mkijijenga juu ya imani yenu takatifu zaidi, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jihifadhi katika upendo wa Mungu, mkitafuta huruma ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa uzima wa milele" (Yuda 20-21). Bibilia imejazwa na ukweli wa upendo wa Mungu lakini nyakati nyingine tunaweza kujiuliza ni kwa vipi Bwana anaweza kutupenda.
Mamilioni ya waumini ambao wameonja upendo wa Mungu hawajawahi kujifunza jinsi ya kuingia utimilifu wa upendo wake. Wanajua mafundisho ya upendo wake - wameisikia yakihubiriwa mara nyingi - lakini hawajui inachomaanisha kutunzwa katika upendo wake.
Yohana 3:16 inasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Ufunuo wa upendo wa Mungu unakuja kwa sehemu kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu tunapozaliwa mara ya pili. Ni wakati mzuri sana unapofahamu ukweli huu na kugundua, "Mungu alinipenda nilipopotea, nikifanywa, mgeni, na alithibitisha upendo wake kwa kumtoa Mwanawe kwa niaba yangu."
Baada ya ufunuo huu wa kwanza, Wakristo lazima wajifunze jinsi ya kutunzwa katika upendo wa Mungu. Baba anapenda watu wake kwa upendo kama huo alio nao kwa Yesu, ambaye ameketi mkono wake wa kulia. Katika sala yake ya mwisho hapa duniani, Yesu alisema, "ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu" (Yohana 17:24). Ni wazo la ajabu sana! Kristo alipendwa sana na Baba kabla ya uumbaji - kabla ya sayari yoyote kuumbwa, kabla ya jua, mwezi au nyota kutokea, kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu.
Kisha Yesu akafuata na sala hii ya kushangaza: "Ili upendo uliyonipenda mimi uwe ndani yao, nami ndani yao" (17:26). Alikuwa akisema, "Baba, najua utawapenda wale ninaowaleta mwilini mwangu kama vile umenipenda." Unaona, kulingana na Yesu, katika macho ya Mungu, Kristo na Kanisa lake ni kitu kimoja.
Jitunze katika upendo mkubwa wa Mungu kwako na itakuwa nguvu yako kupitia vitu vyote unavyoviona maishani.