KUENDELEZA TABIA YA MAOMBI

David Wilkerson (1931-2011)

"Bali wewe unapoomba, ingia chumbani kwako, na ukisha kufunga mlango wako, omba kwa Baba yako aliye katika mahali pa siri; na Baba yako aonaye kwa siri, atakubariki kwa uwazi” (Mathayo 6:6).

Yesu anaposema juu ya kwenda mahali pa siri kumtafuta Baba, anasema juu ya kitu kikubwa sana kuliko kitu kinacho kuwa kalribu ya mwili. Anazungumzia mahali popote ambapo unaweza kuwa peke yake naye katika ushirika wa karibu.

Je! Unayo mahali pa sala? Je! Una tabia ya kujifungania na Mungu? Inawezekana kuwa ndani ya gari lako wakati unaenda kazini au kwenye masomo yako nyumbani. Roho Mtakatifu anakusumbua na roho yako inajibu, "Lazima nizungumze na Baba yangu leo!" Kuwa na tabia ya maombi, mazoezi ya kila siku ya kukusaidiya kuwa mbele za Mungu, ni muhimu kwa ukuaji wako wa kiroho.

Yesu alionya dhidi ya unafiki katika sala. Alichora tofauti kubwa kati ya wale wanaomtafuta Mungu mahali pa siri na wale wanaoomba ili waonekane na wengine kama watakatifu. Wanafiki ni watendaji, watu ambao hujifanya kuwa watakatifu ili kupokea sifa kutoka wengine. Yesu alisema wapo watendaji wengi katika kanisa lake: “Wakati mnapoomba, msiwe kama wanafiki. Kwa maana wanapenda kusimama katika masinagogi na pembezoni za barabara, ili waonekane na watu. Kweli amin, nawaaambia, wamekwisha kupata thawabu yao” (Mathayo 6:5).

Wakristo wengi sana hawafanyi mazoezi ya ajabu, ya ushirika na Bwana kila siku. Wengi wao husali kanisani na milo, na labda na maneno machache ya haraka kwa Mungu kabla ya kulala. Wapenzi wangu, hakuna nguvu kabisa katika kufanya upesi, kuomba kwa ajili ya kuomba. Mungu huona undani wa hali yako na anatamani wewe umtafute kwa moyo wako wote.

Tabia ya kumkaribia Mungu kila siku inasemekana kwa kila mmoja wetu! "Heri wale wanaotii shuhuda zake, wanaomtafuta kwa moyo wote!" (Zaburi 119:2).