KUEPUKA DHAMBI YA MASHAKA

David Wilkerson (1931-2011)

Asafu, Mlawi, alikuwa mwimbaji mkuu na kiongozi wa waabudu wa kifalme wa Mfalme Daudi; kwa kweli, ana sifa ya kuandika kumi na moja kati ya Zaburi. Alikuwa rafiki wa karibu sana na David, na wawili walipenda kuwa katika nyumba ya Mungu pamoja. Lakini, licha ya wito wake mwingi na baraka, Asafu alikiri, “Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka; hatua zangu zilikuwa karibia na kuteleza” (Zaburi 73:2).

Sasa, tunajua Asafu alikuwa mtu mwenye moyo safi ambaye aliamini Mungu alikuwa mzuri. Kwa kweli, alianza hotuba yake katika Zaburi hii kwa kusema, "Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa walio na mioyo safi" (73:1).

Lakini, katika aya ifuatayo Asafu anakiri kwamba alikaribia kuteleza. Kwa nini alitangaza hili? Anabaini kuwa aliwaona waovu wakimzunguka wakifanikiwa wakati walipuuza amri za Mungu na ingekuwa rahisi kwa Asafu kujiuliza ni kwanini Mungu "hakupima vitabu" hivyo kusema.

Je! Hujawahi kujiuliza ni kwanini baraka zinapatikana kwa watu wanaoishi maisha yavurugu? Labda umeona mfanyikazi mwenzako asiyemcha Mungu akilipwa kuriko wewe au jirani yako ambaye hajaokoka anapata vitu vya kimwili wakati wewe unajitahidi sana ili upate mahitaji.

Inaweza kuwa rahisi sana kwa Wakristo wanaoteseka kuingia kwenye dhambi mbaya - dhambi ya mashaka. Unaweza kufikiria, "Nimekuwa ninaishi sawa, lakini uangalifu wangu wote na bidii ya kusoma Neno la Mungu, kusifu kwangu na kuabudu, imekuwa bure. Licha ya hayo yote ninafanya, bado ninaendeleya kuteseka."

Mpendwa, huyu ni wakati ambao lazima uwe mwangalifu. Jaribio lako linapokujilia, unapo huzuni au umekata tamaa, unahitaji kulinda moyo wako dhidi ya kulala katika  mashaka. Usiruhusu imani yako au ujasiri wako kutikiswa. Mungu bado yuko kwenye kiti cha enzi. Ondoa macho yako mbali na majaribu yako, na uweke macho yako kwa Bwana mwenyewe. Mungu atakusaidia kumpenda na kamwe usisinzie katika kutokuamini.

Asafu aliona kwamba alikuwa karibu kuteleza lakini aliendelea kutangaza, "Nimefanya kimbilio kwa Bwana Mungu, ili niweze kutangaza matendo yako yote" (73:28). Na unaweza kufanya vivyo hivyo!