KUFUAT WA NA BABA MWENYE UPENDO

David Wilkerson (1931-2011)

Baada ya Adamu na Hawa kula tunda liliokatazwa katika bustani ya Edeni, walijificha kutoka kwa Mungu walipomsikia akitembea bustani wakati wa kabaridi ka mchana (tazama Mwanzo 3:8). Na baada ya Daudi kutenda dhambi pamoja na mke wa mmoja wa mashujaa wake mkuu, na kisha alipanga kuuawa kwa mtu katika vita ili aweze kuowa mwanamke huyo, tunamwona Daudi alijinowa mwenyewe. Alikataa kwenda kwenye vita na badala yake akajificha ikulu. Alipoteza mapigano yake yote na alikuwa na hofu ya kukabiliana na Mungu na dhambi isiyotubu.

Daudi kamwe hakufikiri alikuwa ameondolewa na dhambi; Kwa upande mwingine, alikuwa mtu mwenye shida sana, mwenye hatia ambaye aliandika kutokana na uchungu wa moyo wake: "Usinitenge na uso wako, wala Roho yako Mtakatifu usiniondolee. Unirudishe furaha ya wokovu wako" (Zaburi 51:11-12).

Katika kesi ya Adamu na Hawa na pia Daudi, baraka nyingi za Mungu zilikuwa wazi, lakini dhambi iliingia. Walijificha kutoka kwa Mungu bila hatia, lakini Baba yao mwenye upendo aliwafuata kutokana na upendo wake mkubwa na akawaleta tena katika ushirika pamoja naye.

Vivyo hivyo, ikiwa unakimbia kutoka kwa Mungu kwa sababu ya dhambi isiyotubu, anaona uchungu wako na huzuni juu ya hilo. Yeye hafurahishwi kwa kukuona ukiwa katika maumivu na atafanya hoja ya kwanza ya kukuunganisha na moyo wake. Anaweza kutuma mtu kukuazibu na kukupinga, kama alivyomtuma Nathani nabii kwa Mfalme Daudi  (angalia 2 Samweli 12:1-15), au anaweza kutumia njia nyingine. Lakini upendo wake kwa ajili yako hautamruhusu kukaa tu na kukuacha uende.

Rehema ya Mungu inanipita kabisa! Lakini wakati umevunjikia mbele yake, ingawa inaweza kuwa ngumu kwa madhara yenye maumivu kutokana na dhambi yako, neema yake inakuwezesha kutoka katika vivuli na kufanya upya ushirikiano wako pamoja naye.