KUHUSIANA NA WATU WA MUNGU
"Namshukuru Mungu wangu kira niwakumbukapo ... kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza injili tangu siku ya kwanza hadi sasa" (Wafilipi 1:3-5).
Paulo anamshukuru Mungu kwa ushirika wa watakatifu; koinonia - kushiriki pamoja - ambao yeye na kanisa la Wafilipi walifurahia wakati walikua wanatembea pamoja kwa imani. Ushirika huu katika injili sio kama mwingine wo wote. Una nguvu kwa sababu umezaliwa chini ya msalaba wa Yesu Kristo. Kupitia yeye, kupitia wanaume wa sehemu mbali mbali, makabila, na lugha zote hukutana kama mwili mmoja.
Tunasoma zaidi: “Kwa maana Mungu ndiye shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote katika ndani ya Kristo Yesu. Na haya ndio maombi yangu kwamba upendo wenu upate kuwa na mioyo safi, bila kosa, katika hekima na ufahamu wote, na maarifa na utambuzi wote, ili mpate kuyakubali yaliyoyaliyo mema; bila kosa mpaka siku ya Kristo” (1:8-10). Paulo alifurahishwa na ushirikiano wa waamini wenzake - walikuwa wa kweli na thabiti tangu siku ya kwanza alipokutana nao. Walikuwa wamewasiliana naye na kumuunga mkono alipokuwa peke yake gerezani, na alishukuru sana.
Paul alikuwa akimshukuru Mungu kwa marafiki zake ambao walikuwa wanaelewana sana kupitia miaka yote. Roho Mtakatifu alikuwa ameunganisha mioyo yao pamoja na walikuwa wamoja katika Kristo. Paulo alitaka upendo wake kwa waumini hawa uwongekeze Zaidi na zaidi.
Vivyo hivyo, leo, Bwana anataka watoto wake wawe katika ushirika, wa kupendana na kusaidiana. Sio tu hili litaimarisha matembezi yetu pamoja naye, lakini jamii ambayo imejengwa kwa musingi wa kibibiliya inaweza kuwa ushuhuda wenye nguvu kwa ulimwengu.
Je! Unajitahidi kuungana katika mahusiano na waamini wenzako? Ninakutia moyo utafute fursa za kuhusiana na watu wa Mungu kwa njia mpya. Sio tu kwamba unaweza kuwapa wengine, lakini wanaweza kutajirisha matembezi yako na Mwokozi - na kwa pamoja, unaweza kuunda kifungo cha imani. Bwana ataweka juhudi zako na baraka zake "ili upendo wako uzidi kuongezeka zaidi."