KUJIAMINI KWA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo wengi wanafahamu mstari huu: "Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15). Tunaona hapa kwamba kuhani wetu mkuu, Yesu, anahisi mateso yetu pamoja nasi. Kwa maneno mengine, Bwana binafsi anaguswa na maumivu yote, kuchanganyikiwa na kukata tamaa tunayohisi. Hakuna kitu tunachokipitia kwamba hakukipitia pia, kwa njia moja au nyingine.

Kwa kuwa tuna kuhani mkuu sana, tunaambiwa, "Basi, tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wamahitaji" (4:16). Tunaambiwa, "Mwokozi wako anajua vizuli sana mambo unaopitia, na anajua jinsi ya kutumikia kupitia neema yake."

Tumesikia zaidi ufafanuzi wa kiteolojia wa neema: upendeleo usiyofaa; wema wa Mungu; upendo wake maalum. Lakini wakati majaribio anakuja, tuna uchaguzi wa jinsi tutakavyoitikia. Katika kitabu cha Ayubu, tunaona kwamba mke wa Ayubu alikasirika na msiba usioonekana ambao walikuwa wanateseka. Yeye kwa upumbavu alimlaumu Mungu na kumwomba Ayubu, "Umukufuru Mungu ukafe!" (Yobu 2:9). Alikuwa anasema, kwa kweli, "Kwa nini Bwana ameshusha msiba usiofikiriwa katika familia hii ya kimungu?"

Lakini hata katika huzuni kubwa na upekee, mtu huyu wa Mungu alisema, "Ingawa Yeye ananiua, bado nitamtumaini" (Yobu 13:15).

Ayubu alikuwa anasema, "Haijalishi majoto haya yanipeleka kwenye kaburi langu, sitaacha kuamini anajua chenye anachofanya. Ingawa sijui kitu chochote kuhusu hili, najua Mungu ana lengo la milele."

Wapendwa, mateso yako ya sasa yanatengeneza kitu cha thamani katika maisha yako kama unapofanywa kuwa mtoaji wa neema.