KUKITIMIZA KUSUDI LAKO KUU
"Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, ikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako" (Matendo. 26:16).
"Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu ... kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaloliita jina wa Bwana wetu Yesu Kristo" (1 Wakorintho 1:1-2).
Aya hizi mbili zinaonyesha kusudi kuu Mungu alikuwa nalo kwa Paulo wakati alipomtokea mala ya kwanza kwenye barabara ya Damasko. Jambo la kwanza Yesu analofanya wakati anapokaribia kubadilisha maisha yetu huonekana kwetu. Labda si kwa fomu ya kimwili, lakini anaanza kufanya utofauti katika ulimwengu na kugeuza ulimwengu wetu upunguke. Baada ya kutuambia "kuinuka na kusimama miguu yetu," huanza kutufunulia kusudi lake jipya.
Kuna kipindi cha muda tunachopewa kuwa duniani (tazama Waebrania 9:27), lakini hatuokolewe tu kwenda mbinguni tunapokufa. Hapana, Mungu ana lengo kwa kila mmoja wetu. Yesu alimupa Paulo kusudi maalum katika maisha yake na tunayaona katika Matendo 26:16 ambayo ni "kuwa mtumishi na kuwa shahidi."
Kama Mkristo, unaitwa kutumikia na kuwa shahidi wa Yesu Kristo kwa wale walio karibu nawe. Mungu amekufanyia nini? Je! Ninkitu gani umeona Mungu ametendea wengine?
Wakati mwingine Yesu alisema, "Basi nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi ... na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa ulimwengu" (Mathayo 28:19-20). Kwa sababu wewe ni mtumishi wa Kristo, yeye ni yuko pamoja nawe daima, akikuwezesha uwe shahidi kwa wale unaotalajia kukutana nao. Hiyo ndiyo kusudi lako kuu!