KUPANDWA NA KUOTA MIZIZI KATIKA UPENDO
"Mwenende katika upendo, kama vile Kristo alivyotupenda ninyi tena akajitoa mwenyewe kwa ajili yetu" (Waefeso 5:2). Mtume Paulo alikuwa akiwahimiza Waefeso hapa, "Yesu anawapenda sana, kwa hivyo tembea kama mtu anayependwa sana na Mungu!"
Waumini wengi Wakristo wamejua juu ya upendo wa Mungu tangu utotoni wakati waliimba wimbo unaopendwa na watoto: "Yesu ananipenda, najua, kwa sababu Biblia inaniambia hivyo." Wengine wanaweza kuwa na maarifa ya kitheolojia juu ya upendo wa Mungu kwa sababu walisikia mahubiri juu yake na hata maandiko yaliyokaririwa. Lakini hawajawahi kuelewa, kwa undani, upendo ambao Mungu anawo kwa ajili yao, wala kupata amani ambayo uelewaji huo unaleta moyoni.
"Ili Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkipandwa na kuota mizizi katika upendo; muweze kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana na urefu, na kimo na upana; na kujua upendo wa Kristo, ambao hupita maarifa; ili mjazwe na utimilifu wote wa Mungu” (Waefeso 3:17-19).
Kupandwa na kuota mizizi hapa inamaanisha "kujenga chini yako msingi wa kujuwa na kuelewa upendo wa Mungu kwako." Kwa maneno mengine, ufahamu wa upendo wa Mungu kwako ni ukweli wa msingi ambao ukweli wote lazima ujengwe juu yake!
Mungu anataka uweze kushika ukweli wa upendo wake na kuufanya uwe msingi wa matembezi yako ya Kikristo. Yeye anataka uweke mikono yako ya kiroho na kusema, "Nitashikilia ukweli huu na kuwa sahihi katika maisha yangu."
Roho Mtakatifu akuwezeshe kuelewa ukweli wa upendo wa Kristo kwako - leo!