KUSHIRIKIANA WUPENDO WA YESU
Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Ni mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka mwende mkuzae matunda" (Yohana 15:16). Kisha haraka aliongeza maneno haya mazuri: "Kwa kuwa matunda yenu yanapaswa kubaki." Maneno haya ya Kristo yanaohusu wanafunzi wake anafaa hata leo. Anasema, kwa kweli, "Hakikisha kwamba matunda yako anadumu."
Neno "matunda" linamaanisha kazi na huduma ya Kristo ambayo wafuasi wake wanafanya hapa duniani. Kama mwamini, wewe umechaguliwa na umewekwa "kwenda ulimwenguni pote na kuhubiri injili ya Kristo" (ona Marko 16:15). Hii inamaanisha kuwafikia wale walio karibu nawe, mahari popote Mungu alipokuita kuishi maisha yako. Yesu pia anasema, "Basi, nendeni mkawafanye wanafunzi" (Mathayo 28:19). Unaweza kufanya hivyo kwa kusimama karibu na aliye okoka karibuni, kwa kuhimiza, kwa kushirikiana ujuzi wako wa Neno.
Mamilioni ya watu wanajaa kanisa kila siku Jumapili, wakiaamini kuwa wako katika fadhili za Mungu tu kwa sababu wanajionyesha kanisani. Hata hivyo, wamejenga mbinu zao wenyewe kuhusu Kristo ni nani – kama mtu alio kama wao wenyewe, aliyefanywa na upofu wao badala ya Neno la Mungu. Wakati unapowasogelea na kuwaambia kuwa ni wenye dhambi japokuwa watubu na kufanya mabadiliko ya kweli katika maisha yao, wanaendelea kung’ania sana. Unakuja na ukweli wa damu ya Kristo, kuzaliwa mpya, kujitenga na ulimwengu, kutembea kwa unyenyekevu na utii. Unakuja kutoa maisha yao kupitia Yesu!
Ni fursa nzuri sana ya kuwasilisha ukweli kwa wengine kuhusu utowaji wa uzima kutoka kwa Yesu. Lakini bila kujali ni kiasi gani cha rehema, neema na upendo wa Kristo, jambo pekee ambalo litatobowa kuta zilizojengwa na watu wagumu ni uwepo wa Yesu. Na hiyo inakuja kupitia kazi ya Roho Mtakatifu.
"Mungu Mwokozi wetu ... ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli" (1 Timotheo 2:3-4). Wakati wowote unaposhirikiyana upendo wa Yesu na mtu, una uhakika kwamba unapitia mapenzi ya Baba yako wa mbinguni.