KUTAFUTA MAPUMZIKO KWA NAFSI ILIYOOGOPA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alikuja duniani kama mtu wa kuwakomboa wanadamu kutoka kwa dhambi zetu na kila aina ya utumwa. Lakini pia alikuja duniani kwa lengo la kutufunulia Baba wa mbinguni.

Aliwaambia wanafunzi wake, "Baba amenituma" (Yohana 5:36). Pia alisema, "Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe ... Siyatafuti mapenzi Yangu mimi, bali mapenzi ya Baba aliyenituma" (Yohana 5:30). Kisha akasema, "Naenda kwa Baba Yangu" (Yohana 14:12).

Yesu alikuwa akisema mambo matatu: "Nilikuja kutoka kwa Baba. Wakati nipo hapa, nitafanya tu mapenzi yake. Hivi karibuni nitarudi kwa Baba." Uzima wote wa Yesu - kuja kwake duniani, kusudi lake wakati alikuwa hapa, na kurudi kwake mbinguni - ilikuwa juu ya kumfunua Baba wa mbinguni.

Yesu akawaambia Mafarisayo, "Angalia maisha yangu, huduma yangu, miujiza yote na matendo mema nafanya, na mtaona Baba wa mbinguni. Kila kitu ninachofanya ni kutafakari kuwa yeye ni nani na hayo yote ni maana ya kumfunulia yeye."

"Nimekabiziwa vyote na Baba yangu, wala amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amujuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana anapenda kumufunulia" (Mathayo 11:27).

Yesu anasema kwamba haiwezekani kwetu kujua Baba ni nani isipokuwa Yesu amtufunulia kwetu. Halafu, anaongeza katika mstari unaofuata: "Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, name nitawapumuzisha" (11:28).

Yesu anatuonyesha kwamba ikiwa tunataka kupumzika kwa nafsi yetu, na mwisho wa kujitahidi kuandani, tunapaswa kuwa na ufunuo wa kujua ni nani Baba. Lazima ujue kwamba una Baba mbinguni ambaye anakujali wewe! Hakuna mtu anayepokea ufunuo huu isipokuwa kutoka kwa Kristo na katika kila kitu anachofanya na kusema, anatuonyesha moyo wa Baba.