KUTAWALA KWA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Katika Hesabu 13 na 14, tunapata lugha na ufafanuzi wa imani ya kweli na kutokuamini. Wapelelezi kumi ambao walikuwa wamekwenda kwenye ardhi waliporudi na ripoti ya kile walichokiona. "Tulifika katika nchi ambayo uliyotutuma, na hakika kweli ni nchi yenye maziwa na asali, na haya ndio matunda yake. Lakini watu wakaao katika nchi ni wenye nguvu nyingi; na miji ina maboma na ni makubwa sana” (Hesabu 13:27-28). Kwa hivyo ripoti hiyo upande umjoa ilikuwa nzuri na upande mwingine ilikuwa sio nzuri.

Watu walishtuka na kupiga kelele kwa woga na kutokuamini, "Hatuwezi kwenda kupingana na na hawo watu, kwa kuwa wana nguvu kuliko sisi" (ona 13:31). Lakini Kalebu, na sauti tulivu ya imani, ilikuwa na njia nyingine: "Tuende mara moja, tukaimiliki, kwa maana tunaweza kulishinda" (13:30).

Kusanyiko lote lilijiunga pamoja, nakusema, "Twende tena Misri na utumwani. Hatuwezi kuifanya hiyo Nchi ya Ahadi. Kuna maadui wengi wenye nguvu mno” (14:1-4). Lakini tena, imani inazungumza kupitia Yoshua na Kalebu: "Ardhi ambayo tumepitia ili kuipeleleza ni nchi nzuri sana ... [Bwana] atatuleta katika nchi hii na ataitupatia sisi, nchi ambayo inamwagika maziwa na asali" (14:7-8).

Mungu anataka kujua kilicho moyoni mwako kama mwamini wa kweli. Je! Ni hofu ya wenye nguvu nyingi na hamu ya kurudi Misri? Anataka watu ambao watatumia imani kwa kubomoa kila kitu kinachowazuia kutoka kwa utimilifu wa Yesu.

Adui hana nguvu ya kuwazuia watu wa Mungu kutoka kile anacho kwa ajili yao. Shetani anaweza kuwa anatumia fujo kubwa la shida dhidi yako hivi sasa - sio kukuweka chini, bali kukuweka nje. Kuzimu yote inakupinga ili kukuzuia usiende kwenye utimilifu wa Kristo, mahali pa kupumzika, maisha ya kujiamini na matembezi ya amani chini ya ufalme wake.

Ruhusu imani yako itawale na kutangaza, "sitaogopa kile mwanadamu anaweza kufanya. Adui zangu hawana nguvu, kwani Mungu yuko pamoja nami. Nitaingia katika kile alichonacho kwa ajili yangu!"