KUTOJUA NGUVU ZA ROHO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mara nyingi tunaweza kuwa na kitu muhimu bila kutambua kikamilifu thamani yake au umuhimu wake. Hadithi inayosemwa ya mkulima aliiolima shamba lake ndogo kipindi cha maisha yake yote, akitengeneza aridhi yenye majiwe mwaka baada ya mwaka. Wakati wa kifo chake, shamba lilipitishwa kwa mwanawe ambaye aliendelea kulilima - lakini mtoto huyo aligunduwa  kusanyiko la dhahabu iliyo kwenye udongo. Chamba lilikuwa limejaa dhahabu na mara moja akawa mtu tajiri. Hata hivyo utajiri ulikuwa umepotea wakati wa baba yake, ingawa ilikuwa vigumu yakuwa kwenye ardhi maisha yake yote.

Kwa hiyo ni pamoja na Roho Mtakatifu, wengi wetu wanaishi kwa ujinga wa kile tulicho nacho, chenye nguvu ambazo hukaa ndani yetu. Wakristo wengine wanaishi maisha yao yote kufikiri kuwa na Roho Mtakatifu, lakini bado hawajampokea kwa ukamilifu na kwa nguvu. Yeye hatimizi kazi ndani yao milele aliyotumwa kufanya.

Waumini wengine hutafuta Roho Mtakatifu peke yao wakati wa shida na wanataka aonyeshe nguvu zake. Wanatarajia kuwa atashuka na kuondosha matatizo yao. Lakini Petro anasema kwamba sio kweli kuhusu Roho. Kulingana na yeye, tuna dhamana ndani yetu: "Nguvu zake za kimungu zimetupatia vitu vyote vinavyohusu maisha na utukufu kutoka kwa Mungu" (2 Petro 1:3).

Kwenye Mto wa Yordani, Yohana Mbatizaji aliwaambia Mafarisayo, "Mimi ninabatiza kwa maji, Katikati yenu amesimama yeye msiyemujua ninyi" (Yohana 1:26). Viongozi hao wa kidini walimwona Yesu kwa mwili, na wakamsikia akisema, lakini hawakuelewa ni nani. Hawakujua kuhusu nguvu na utukufu wake. Vivyo hivyo, Yesu alimwuliza mwanafunzi wake mwenyewe, Filipo, "Nimekuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, lakini hajanijua Filipo?" (Yohana 14:9).

Je! Nikipindi cha muda gani umeshuhudia kwamba umejazwa na Roho Mtakatifu? Amekuwa na wewe miaka mingi na bado hujui yeye? Yeye ndiye Ule anatuleta kupitia nyakati ngumu na ushuhuda wa uvumilivu wa furaha. Ushuhuda wetu mkuu duniani ni kuwa Mkristo ambaye alieweka kila mzigo wake kwa Roho Mtakatifu.