KUTOROKA UWEZO WA KUWA KWENYE UPWEKE

Nicky Cruz

Je! Mkristo anaweza kuwa peke yake? Mhubiri aliyejulikana Billy Graham mara moja alisema kuwa kupitia miaka yake mingi ya kuwasiliana na watu ulimwenguni pote, kwa maoni yake, upweke ni tatizo kubwa linalokabiliana na wanadamu. Inadharia hatupaswi kuwa peke yetu kwa sababu Yesu Kristo, ni Rafiki kuzidi marafiki wote, alisema, "Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa" (Waebrania 13:5). Yeye anaishi ndani yetu na tuna rasilimali za kucholewa ambazo wa sio kuwa Wakristo hawajui chochote.

Pili, tuna utambulisho wa kifamilia, kwa kuwa tumekuwa "kuzaliwa tena" katika familia ya Mungu na tuko watoto wake kama ndugu na dada ndani ya Kristo. Hata hivyo, Wakristo wanapambana na hisia peke yake. Katika jitihada yangu mwenyewe ya kutoroka upweke, nimepewa sheria za chini ambazo mimi hufanya kazi kwa daima:

  1. Badala ya kutafuta watu ambao unaweza kuamini, elekeza macho yako kabisa kwa Mungu, ambaye peke yake ndie wakuaminiwa. Kwa kufanya hivyo, unaacha kutarajia zaidi kutoka kwa wanadamu kuliko wanavyoweza ku kusaidia.
  2. Kuchukua muda wa kila siku kuwa peke yake pamoja na Mungu, bila kujali shida au ratiba. Omba juu ya tatizo lolote, iwe kubwa sana. Biblia inasema, "Msijisumbue kwa neno lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kshukuru, haja zenu na zijurikane na Mungu. Na Amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu " (Wafilipi 4:6-7).
  3. Jifunze kusema hapana. Ikiwa una tabia ya kuwa "workaholic" (maana kwamba furaha yako katika maisha yako ni kazi tu), kubali hilo na uanze kulishughulikia hilo. Kuondoa maisha yako kutoka kwenye shughuli zisizohitajika ambazo huibia muda wako wakuwa pamoja na Mungu, muda wakuwa na familia, wa kushiriki katika kanisa, na burudani muhimu.
  4. Badala ya kukaa daima ndani ya matatizo yako, endea mtu mwingine kwa urafiki rahisi. Unaweza kupata kitu kikubwa zaidi kuliko kile unachotoa.

Ingawa bado unaweza kuwa na upweke, Yesu ndiye chanzo cha yale yote unayohitaji.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza  ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka ( Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).