KUUZWA WEWE WOTE KWA AJILI YA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana akamwambia Petro, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate" (Mathayo 16:24).

Kwa wazi, kuwa katika kanisa la Yesu maana yake ni zaidi tu ya kumwamini. Wakristo wengi leo "walipiga kura kwa ajili ya Yesu," lakini kisha wanatembea mbali na kusahau yote juu ya utawala wake kuhusu maisha yao. Bwana wetu anaweka wazi kuwa mali yake inahusisha kuishi maisha ya kujikana na kuchukua msalaba. "Yeyote asiyechukua msalaba wake na kunifuata hanistahili" (Mathayo 10:38).

Yesu anasema, "Kama wewe uko ndani ya kanisa langu, basi uwe tayari kuteswa na kuzalauliwa ikiwa unanjaa na kiu vya kunitafuta. Na uwe tayari kujikana umaarufu wote, kukubalika na kutafuta furaha ya duniani. "Ukweli ni kwamba kanisa la Kristo halijawahi kamwe kukubaliwa na ulimwengu na halitakubaliwa kamwe. Watu wenye kuwa karibu na wewe hawatakuwa vizuri na wanataka kujitenga na kampuni yako. "Heri ninyi watu watakapowachukia, na wakuwatenga, na kuwashutumu ... kwa ajili ya Mwana Damu" (Luka 6:22).

Yesu anatuonyesha njia inayoongoza kwa utimilifu wa kweli: "Na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona" (Mathayo 16:25). Kwa maneno mengine, njia pekee utaopata kuhusu maana ya maisha ni kuuzwa wewe wote kwa ajili ya Yesu. Kisha utapata furaha ya kweli, amani na kuridhika. Kristo anatuambia, "Unapokuja kwangu, lazima ufe kwa nafsi yako, kwa kutokuwa mtu wa kiMungu na kwa mimi tu. Kwa imani utazikwa pamoja nami, lakini nitakufufua katika maisha mapya!"

"Ni Roho ambaye hutoa uzima; mwili haufai kitu. Maneno ambayo nawaambieni ninyi ni roho, na ni uzima" (Yohana 6:63). Maneno tu ya Yesu yanaweza kuzalisha uzima na tunapaswa kuyatumiya kama tunavyoweza kula na kunywa - kwa kusoma kila siku Neno la Mungu na kutumia muda kwa kuwa mbele yake.