KUVUTIWA NA UPENDO WA YESU

Gary Wilkerson

"Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko Efeso, na wanaomwamini katika Kristo Yesu: Neema iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo" (Waefeso 1:1-2). Paulo alikuwa mteule wa Mungu, aliyeitwa kutoka kwa maisha aliyokuwa akiishi na kufanywa mtu wa tofauti. Kwa kusema watakatifu hapa, anaenda katika baraka ya muda mrefu, akiongea kila kitu kilicho moyoni mwake juu ya ukuu na wema wa Yesu (ona aya 3-14).

Hata ingawa Paulo alikuwa mtu mwenye kuwa na elimu, hakujaribu kumvutia mtu yeyote na ufahamu wake, kama wanatheolojia wakati mwingine hufanya. Alikuwa akielezea kilio cha moyo wake, shauku yake kubwa kwa Mungu na yale ambayo alikuwa amemfanyia. Na alikuwa akimtukuza Baba!

Katika Matendo sura ya 9, simulizi la muujiza ambao Mungu alifanya katika maisha ya Paulo linatupatia habari kidogo kwa nini alimwinua Kristo kwa shauku na utakatifu, na kwa faida . Hii haikuwa theolojia tu kwake, sio mafundisho kavu ya kujadiliwa, lakini hii ilikuwa ukweli - kitu ambacho Yesu alitimiza ndani yake kibinafsi. Kama vile Paulo alivyokuwa akiamini kuwa alikuwa akifanya kazi ya Mungu wakati alikuwa ametokana na imani yake ya zamani – kutowa nje vitisho kutoka kwenye moyo wake uliojaa chuki dhidi ya wanafunzi wa Kristo - sasa alikuwa amebadilishwa kabisa, amejitolea, na alivutiwa na upendo wa Yesu, Mkombozi wake.

Paulo alikuwa amejawa na kiburi wakati Yesu aliingia na akabadilisha kitambaa chake. Mwangaza wa mbinguni ulipomfunika wakati alipokuwa anatowa nje vitisho dhidi ya wafuasi wa Kristo, na alikuwa ameangushwa chini – na kuwa kipofu. Akatoka kwenye mkutano huo wa kimungu uliojazwa na ushuhuda wenye mwotomwoto wa upendo na neema ya Yesu Kristo.

Paulo anasema, "Neema iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu." Je! Maisha yako yameelekezwa chini na kuanza kozi mpya? Je! Umegundua neema na amani ya Mungu maishani mwako?  Angalia jinsi ilivyo ajabu kujua kuwa ni zawadi ya bure kutoka kwa Baba yako, na zawadi yako kwa njia ya Yesu Kristo.