LAKINI NITAAMINI MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mwandishi wa Waebrania anatuambia, "Kwa kuwa hamna kuwani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15).

Wakristo wengi wanajua mstari huu; unatuambia kwamba kuhani wetu mkuu, Yesu, anahisi mateso yetu sawa na sisi. Yeye binafsi huguswa na maumivu yetu yote, na kuchanganyikiwa pamoja na kukata tamaa ambayo hutukuta. Kwa kuwa tuna kuhani mkuu sana, tunaambiwa, "Basin a tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wahitaji" (4:16). Tunaambiwa, "Mwokozi wako anajua mambo unayopitia na anajua vyema jinsi ya kutumikia neema yake kwako." Tunapokuwa na haja kubwa, tunawezaje ''kupata neema,'' kama Waebrania wanavyoonyesha?

Wakati janga linapopiga unapaswa kuchaguwa: ama kumwamini Mungu au kumulaumu. Wakati Ayubu na mkewe walipitia kwenye hali maya ya kupoteza familia zao na maafa ya hali yake ya kimwili, walichagua athari mbili tofauti kabisa. Mkewe alikasirika na kuhukumu Mungu kwa upumbavu, hata akamwomba mumewe "Umkufuru Mungu, ukafe" (Ayubu 2:9).

Ayubu pia aliomboleza sana na alikuwa na maumivu makubwa ya kimwili, lakini alimwamini Mungu katikati yahayo yote. Alisema, "Sielewe kitu chochote kinachoendelea, lakini hata akiniua, bado nitamtumaini" (Ayubu 13:15). Ayubu alikuwa anasema, kwa kweli, "Haijalishi kama maji haya yanipeleka kwenye kaburi langu. Nitatoka nje kumwamini Bwana na sitakuacha kuamini kwamba anajua anachofanya. Ana lengo la milele na nitamtumaini kwa pumzi yangu ya mwisho."

Nini imani kubwa katika moyo wa Ayubu! Na ukweli wa ajabu ni kwamba imani hiyo kwa Baba yetu mwenye upendo inaweza kuwa yetu ikiwa tunamwamini.