MAFANIKIO YA MOYO WA MTUMISHI
Paulo, aliyekuwa anajulikana kama Sauli wa Tarso, alikuwa njiani yake kwenda Damaski na kundi ndogo la kijeshi ili wafanye ili wateke Wakristo, kwa kuwaleta Yerusalemu, ili wawafunge na kuwatesa. Lakini Yesu alimtokea Sauli kwenye barabara ya kuelekea Damasko, nakumfanya kuwa kipofu. "Naye [Sauli] akawa siku tatu bila kuona, hali, wala kunywa" (Matendo 9:9).
Katika siku hizo tatu, mawazo ya Sauli yalikuwa akifanyiwa upya. Alitumia muda wote katika maombi ya mfurulizo, akizingatia maisha yake ya zamani, na akaanza kudharau kile alichokuwa. Ndipo wakati huo Sauli aligeuka Paulo.
Mtu huyu alikuwa na kiburi sana, ilikuwa amejaa jitihada zisizofaa. Alitaka kibali cha watu wengine wa dini wenye nguvu sana, lakini akasema, "Naam, Zaidi ya hayo nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote na kuyahesabu kama takataka, ili nipate Kristo" (Wafilipi 3:8).
Paulo alikuwa mtu ambaye angeweza kusema, "Mimi apo mwanzo nilikuwa mtu, wenzangu katika baraza, ikiwa ni pamoja na Mafarisayo wenzangu, walinitazama. Nilikuwa nikipanda ngazi, na nilikuwa nikiitwa mtu mtakatifu, mwalimu mkali wa sheria. Nilikuwa na sifa katika nchi na sikuwa na hatia machoni mwa watu.
"Lakini wakati Kristo alipo nitokea, kila kitu kilibadilika. Kujitahidi, kushindana - kila kitu nilichofikiri kilichofanya maisha yangu kuwa na maana – ilikuwa ni kujitowa. Niliona kwamba nimemkosa Bwana kabisa."
Paulo alifikiri matarajio yake ya kidini - bidii zake, ushindani wake wa kiroho, kazi zake, kufanya mambo kwa bidi – kama hayo yote ni mambo ya haki. Lakini Kristo alimfunulia kwamba ni mwili wote, wote kwa ajili ya nafsi. Kwa hiyo, Paulo alisema, "Niliweka kando kila tamaa ya kufanikiwa na kutambuliwa na nimeamua kuwa mtumishi" (tazama 1 Wakorintho 9:19).
Ikiwa unataka kuacha ubinafsi, tamaa na sifa za kidunia, nakuhimiza kufuata mfano wa Paulo. Sijui njia nyingine ya mafanikio ya moyo wa mtumishi, isipokuwa kupitia maombi.