MAHITAJI YA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati Mungu anasema kwa wanadamu, "Amini," anadai kitu kinapita zaidi ya sababu. Imani inakuwa isiyo na maana yote na ufafanuzi wake unahusiana na jambo lisilo na maana. Fikiria juu yake: Waebrania anasema kwamba imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarijiwayo, ushahidi wa mambo yasioonekana (ona Waebrania 11:1). Tunaambiwa, kwa kifupi, "Hakuna kitu kinachoonekana au ushahidi wowote wa wakati wote." Hata hivyo tunaombwa kuamini.

Ukweli ni kwamba, sisi sote tunakabiliwa na hali ngumu katika maisha haya. Hata hivyo naamini kama tunaweza kuelewa asili ya imani - asili yake isiyo na maana, isiyo eleweka - tutapata msaada tunahitaji ili tuweze kuwupitia.

Hebu tuzingatie Ibrahimu. Mungu akamwambia, "Simama, ondoka, na uache nchi yako." Kweli Ibrahimu aliuliza, "Nitaenda wapi, Bwana?" Lakini Mungu amemwambia aende!

Hii haikuwa ya mantiki; kwa kweli, ilionekana kuwa haina maana. Ikiwa mume akirudi nyumbani na kumwambia mke wake wanahama mara moja, angekuwa na maswali ya kila aina. Wapi? Kwa nini? Vipi? Lini? Na haikubaliki kwake kwamba hataki kuwa na majibu.

Lakini Ibrahamu alikuwa amesikia kutoka kwa Mungu! "Kwa imani Ibrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka akaenda mahari asiojua" (Waebrania 11:8). Ibrahimu alichukua familia yake na kuondoka, bila kujua mahari pakuishia. Yote aliyojua ni kwamba alikuwa na neno fupi kutoka kwa Mungu kwenda na uhakika kwamba hakuna madhara ingemufanya kitu.

Imani ilidai kwamba Ibrahimu asifanye kitu chochote zaidi ya ahadi. Alitii na Neno linasema, "Akamuhesabia jambo hili kuwa haki" (Mwanzo 15:6).

Bwana anakuambia, kama alivyomwambia Abrahamu, "Nitawapa Neno langu na nitajibu kilio chako." "Maskini huyu aliita, na Bwana akamsikia ... uso wa Bwana ni juu ya watenda haki na Masikio yake huelekea kwa kilio chao" (Zaburi 34:6, 15). Mwamini leo ili kukupa kile kili unachohitaji.