MAISHA AMBAYO SHETANI HAWEZI KUHARIBU!

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alipokuwa amelala kimya ndani ya kaburi baada ya kusulubiwa kwake, Shetani na vikundi vyake vilikuwa vinaunguluma. Walifikiri kwamba wameshinda ushindi usiogeuzwa lakini kila wakati, mpango wa Mungu ulioamuliwa ntangu zamani ulikuwa ukiwekwa katika hatua - mpango wa uzima wa ufufuo!

Bwana alimtuma Roho Mtakatifu ndani ya shimo ndefu ya kifo na huko alimfufua mwili wa Yesu, akamfufua kutoka kwa wafu. Kisha nje ya kaburini akawa Mwokozi wetu aliyebarikiwa, kwa njia ya jiwe kubwa. Naye akainuka na ushuhuda huu:

"Mimi ndiye aliyeishi, aliekufa; na tazama, mimi ni hai milele. Amina. Na nina funguo za Hades na Kifo" (Ufunuo 1:18). Kristo alikuwa anasema hapa, "Mimi ndiye aliye na uzima wa milele. Nilikufa, lakini angalia, mimi ni hai, sasa na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu!"

Wakati Yesu alipokuwa anatembea kutoka eneo la kifo, akawa ufufuo na maisha, sio kwa ajili yake mwenyewe bali kwa wote ambao wangemwamini tangu siku hiyo. Yeye ametuletea uzima wa ufufuo kabisa kabisa kupita uwezo wa nguvu za kifo.

Kwa sababu hii, hakuna sababu yoyote ya Mkristo kuogopa kifo au kuiona kama adui. Bwana wetu ameshinda kabisa: "Mungu alimfufua, akiufunga uchungu wa mauti" (Matendo 2:24).

Ikiwa ulimpokea Yesu kama Mwokozi wako na Bwana, basi anaishi ndani yako kama nguvu kuu ya ufufuo. Na uwezo ule ule wa ufufuo ambao umemtoa kutoka kaburini utakuwezesha pia. "Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani. Je! Hamujijui wenyewe kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?" (2 Wakorintho 13:5). Ndani yako yote ambayo ni ile iko ndani ndai ya Kristo, uwezo wa wuzima wenye nguvu ambayo Shetani hawezi kuharibu!