MATUMAINI YETU KAMA VITU VYOTE VINAUMBAUMBA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu anatuambia nini tunachotakiwa kufanya wakati tunapoanza kuona uchungu duniani: "Tena kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mabo yatakaoupata ulimwengu kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mkubwa. Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu utakuwa unakaribia" (Luka 21:25-28).

Angalia Kristo anasema, "Unapoanza kuona mambo haya yakitokea, kisha angalia, inueni vichwa vyenu." Hii inaonyesha mambo Zaidi yatakaotokea na kuwa makali zaidi. Kwa hiyo, sasa ndio wakati wa kuweka mioyo yetu - kumkaribia Bwana - na kuimarisha imani yetu katika Neno lake.

Je, ni imani gani tunayosimamia? Ni kwamba shetani hawezi kutuumiza. Habari zenye machafuko haziwezi kutuumiza. Wadanganyifu wote wanaoongozwa na pepo mbaya watapuliziwa mbali kama pumba, na tunakwenda kumuona Kristo akija katika utukufu wake. Hii ndiyo inatuwezesha kusema katika nyakati mbaya, "Kuishi au kufa, mimi niko upande wa Bwana. Yeye ndiye mwenye nguvu juu ya yote yanayotuzunguka."

Katikati ya haya yote ya "mtetemeko wa vitu vyote" duniani, tahadhari ya Bwana inalenga wapi? Je, wasiwasi wake mkubwa uko juu ya matukio ya Mashariki ya Kati au misukosuko kutoka sehemu nyingine za ulimwengu? Hapana! Biblia inatuambia kwamba maono ya Mungu ni kufunza watoto wake. "Tazama, jicho la Bwana liko juu ya wale wamchao, kwa wale wanaotegemeya fadhili zake" (Zaburi 33:18).

Baba yetu anajua kila harakati duniani, kwa kila kitu kilicho hai, na bado macho yake anazingatia hasa ustawi wa watoto wake. Anaweka macho yake juu ya mahitaji ya kila mmoja wetu. "Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio chao" (Zaburi 34:15).