MATUMAINI YETU KATIKA DHORUBA IJAYO

David Wilkerson (1931-2011)

Hakuna mtu anataka kusikia habari mbaya na kanisa leo sio halijienge kwa hilo; kanisa la Amerika linaonekana kuwa linajihusisha na ujumbe wa "kujisikia vizuri". Tabia hii imeenea katika vitabu na magazeti mengi tunayopata katika maduka ya vitabu vya Kikristo. Ni karibu kama viongozi wetu wanasema, "Pumzika! Mungu ni Baba yetu na sisi ni watoto wake wote na tunatakiwa kuwa na wakati mzuri."

Dhoruba inakuja na Mungu anataka watu wake wawe tayari. Itakuja kama mwizi usiku, kuleta italetahofu ya ghafla na kutoamini. Unaweza kuwa unafikiri, "Ikiwa msiba unapiga, basi acha uje! Mimi niko mikononi mwa Mungu, hivyo Yesu ataniona kupitiya hayo."

Kabla mbele ya kifo chake na kufufuliwa kwake, Yesu aliangalia mbele ya dhoruba inayokuja yenye kutisha. Aliona kuwa hapo awali, Yerusalemu ingezungukwa na majeshi yenye nguvu, hekalu lingeangamizwa, jiji hilo lingeteketezwa chini, na jamii yao yote ingeanguka!

Sasa, Yesu alikuwa mfano mzuri wa upendo wa Mungu na alilia juu ya jamii yake kwa sababu aliona kilichokuja. "Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, amabayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote" (Mathayo 24:21-22).

Ikiwa tunafikiri juu yake, tunaona kwamba siku ya Yesu ilikuwa sawa na yetu: amani, utulivu na mafanikio. Kama vile Yesu alivyoonya kuwa dhoruba ilikuwa inakuja, yeye aliendelea kutafuta maeneo penye siri pa kujifungania pamoja na baba yake. Aliamini kabisa kwamba Mungu alikuwa pamoja naye, Yesu alijua kwamba alikuwa katika udhibiti kamili!

Wapendwa, ikiwa tunakwenda kukabiliana na dhoruba inayokuja, tunahitaji kuwa tayari ili pasiwe kitu kinachovunja roho yetu. Tunaweza kufanya hivyo tu kwa kutumia muda katika uwepo wa Baba - jifunganiye ndani yake mpaka tutakapomshawishi kabisa kuwa yeye yuko upande wetu wa kulia.

Katika uwepo wa Yesu tunapata furaha, tumaini na kupumzika - yote tutakayohitaji!