Najua Kwa Hakika

“Ninamjua Yeye niliyemwamini na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana Kwake hadi siku ile. (Timotheo wa Pili 1:12, my italics). Haya ni maneno ya mtu aliyekuwa mwisho wa maisha yake, Mtume Paulo alikuwa akimueleza mwanafunzi wake, Mtumishi mchanga aliyekuwa mafunzoni, Timotheo. Katika barua hii, Paulo alimnong’onezea Timotheo maneno haya mazito. “Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda” (Timotheo wa Pili 4:7). Ingawa Paulo aliamuandikia Timotheo, maneno haya yana umuhimu kwa kila Mkristo anaye pitia mateso. Tafakari: wakati huu wa majaribu – alipokuwa kifoni – Paulo alikua na hakika kamili kuhusu Upendo wa Mungu kwake. Na tena, aliamini kabisa uwezo wa Bwana Mungu “kukilinda kile nilichokiweka amana Kwake” ingawa ushahidi wote ulikuwa kinyume na mawazo haya.

Wapendwa, Mawaidha ya Paulo ni yetu sote tulio kumbwa na vita vya kiroho, tunao pitia shida kama majeshi wazuri. Paulo angewezaje kuongea kuhusu uaminifu wa Bwana katika majaribu? Ni nini haswa alichokuwa na hakika nacho kumhusu Bwana Mungu iliyo zaa Imani kiasi hiki? Paulo hakusema ni nini “alichokiweka amana Kwake (Mungu) hadi siku ile”. Tunaweza tu kubahatisha ni nini haswa alichomkabidhi. Walakini, kama Paulo, nasi inatubidi tuwe na Hakika kamili katika Imani kwamba Bwana Mungu anaweza kuviweka vile tulivyo mkabidhi. Kukumbana na majaribu ya nyakati hizi, inatubudi tuwe na hakika kamili kuhusu Mungu wetu.

1. Lazima Tuwe Na Hakika Kwamba Hakuna Kile Kinachoweza Kututenganisha Na Upendo Wa Mungu Ndani Ya Yesu Kristo.

Paulo aliandikia Warumi:

“Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:38–39). Kabla ya kutoa Tamko hilo, Paulo aliuliza swali: “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga?...Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda” (Warui 8:35, 37). Ni wazi kwamba Paulo kupitia maswali haya anaonesha kuelewa makusudi ya Shetani siku hizi za Mwisho: Kuzuia watoto wa Mungu kutembea katika Upendo wa ajabu. Lakuhuzunisha ni kwamba, maelfu ya wale walio Kanisani ni vipofu kwa mitego ya muovu. Wengi wanaishi wakiwa hawana habari kuwa wamefungiwa kujua na kufurahia Upendo wa Mungu kwao.

Usinielewe vibaya, hatufaye kamwe kumuogopa yule Muovu. Lakini kama hatuelewa mbinu zake za kupingana na Imani yetu, tutaendelea kushindwa maishani. Paulo alijua umuhimu wa kuziweka wazi mbinu za Shetani. Tunapoweza kuzifahamu hizo mbinu zinazopinga Imani yetu, ndiposa twaweza kusema kama Paulo, “Ninaamini kua - hakuna uongo wala mashtaka – yataweza kunitenganisha na Upendo wa Mungu, iliyo ndani ya Yesu Tristo.” Lazima tuelewe kua Shetani ana nia ya kufunga kila huduma inayo ongozwa na Roho Mtakatifu, kuwashurutisha Wakristo wakiroho siku hiz za Mwisho. Analenga kila Muumuni aliye simama imara kupingana na ufamle wa giza, sio tu wachungaji.

Miaka michache sasa nimekuwa na msukumo moyoni kwamba masaibu ya wateule wa Mungu siku za leo hayajawahi kuonekana katika historia ya Kanisa la Tristo. Wateule wa Mungu wamekuwa wakipitia masaibu mengi. Waibrania 11 inaeleza haya. Na sasa, Neno linasema, Shetani ameinuka kinyume na Kanisa kwa sababu wakati wake ni mfupi. “Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!’ (Ufunuo 12:12). Kurudi kwake Yesu uko Mlangoni, akiwa na hasira nyingi, Muovu na adui wa Nafsi zetu amekuja kudanganya hata Wateule wa Mungu. Hata sasa, majeshi ya watumishi wa Shetani yanaendelea kuvunja moyo na kuwaaharibu wateule wa Mungu. Paulo atoa ushuhuda kuhusu mateso aliopitia maishani akisema, “Maana tulitaka kuja kwenu, hasa mimi Paulo, nilitaka kuja tena na tena, lakini Shetani akatuzuia. (Wathesalonike wa Kwanza 2:18).

Katika Karne iliyopita, T. Austin Sparks aliandika kuhusu vita vya Shetani siku hizi za Mwisho. Mtumishi huyu wa Mungu aliona mambo mengi yakizuiwa, yakishindikizwa chini, yakibanwa na Shetani, kana kwamba maelfu ya Wakristo wameshindwa kutekeleza huduma zao….kwa sababu ya Uzuizi wa Shetani. Kama Paulo hapo mbeleni, Austin-Sparks alionya watu wa Mungu wawe makini kwa mbinu za Shetani. Aliwasihi waumini waombe kumsihi Mungu amshushe Shetani kutoka pale mahali ambapo “anawashtaki waumini”. Ninaamini Maombezi kama hayo ni ya kweli kwa Muumini yeyote alione Uzuizi wa Shetani. Waumini hawa wanajua kamili vita inayowakumba wale wanao ongoza wengi katika njia safi ya Kristo.

Nimekuja Kuamini Kwamba Lengo Kuu La Shetani Ni Kuzuia Waombezi Wa Mungu.

Nini basi maana ya Muombezi? Huyu ni yule ambaye hubeba mizigo ya wengine kwa Maombi. Mtumishi kama huyo hachoki Kuombea Kanisa la Kristo au yeyote yule Bwana ameweka kwa Roho yake. Enzi zote, Mungu ameweka Waombezi mbele ya Vita, kufanya vita kinyume na nguvu za giza. Waombezi hawa leo wanapatikana katika nchi zote duniani. Kuna sababu wanaitwa “Majeshi ya Waombezi”. Wengi wanaotuandikia wanaeleza vita katika Maisha yao wenyewe. Muombezi aliye na miaka 91 alisema haya: “nasikia kuisha nguvu, baada ya utumishi wangu wa miaka mingi kwa Mungu nikipigana kila aina ya vita. Niko mnyonge mwilini baada ya Miaka mingi ya shida – nikishughulikia shida na masaibu ya wengine….tangu nilipokuwa miaka 4, nimewapenda na kuombea wengine. Nimekuwa Muombezi miaka hii yote….ninaichukua na kurejeshi umilki wangu kila mara Shetani anajaribu kuiba, kwa kuomba kiroho… na ninapokea nguvu mpya.” Maisha yote, mtumishi huyu alichukulia maanani mawaidha ya Yuda: “Lakini ninyi wapenzi, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu. Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia kwa furaha rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ili awalete katika uzima wa milele.” (Yuda 20 – 21). Ujumbe kwa wale wale wapiganao vita vya kiroho ni wazi: Jijengeni katika imani yenu. Jilindeni katika upendo wa Mungu. Tafakari kwamba Yuda atia nguvu Ujumbe wake kwa kutusihi tuombe katika Roho Mtakatifu. Haiwezekani kamwe kujenga Imani kupitia nguvu au uweza wa kimwili. Bila Roho Mtakatifu, hatuweza kuwa kamili katika ufahamu wa upendo wa Mungu kwetu. Hatuweza kukabidhi nguvu za giza pekee yetu. Hatuweza hata kuinua ngao za Imani kuzima mioto ya kuzimu kwa kujaribu kuelekeza akili zetu. Tuna muhitaji Roho wa Mungu anaye tuweka Nguvu katika kila hali.

Nyakati hizi za shida, kunakili Neno pekee haitoshi. Najua mtumishi ambaye ufahamu wake katika Neno la Mungu lilikuwa maradufu aliitwa “Biblia inayotembea.” Mtu huyu angeweza kunakili vitabu vizima kutoka kwa Bibilia. Alipokumbwa na masaibu makuu, alianguka katika Imani. Kama Paulo anavyo nena, “kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima. (Wakorintho wa Pili 3:6). Ni huzuni kwamba wakristo wengi wanaokiri kujazwa na Roho hawamrudii Roho Mtakatifu wanakumbwa na shida. Hawaelewi Amani na Utulivu wake, wakati kazi yake kuu ni kutupatia vitu hivi. Waumini hawa bado hawajajua kumtegemea Roho, labda ni kwa sababu hawajajua kwa hakika kuwa wanamuhitaji.

Shida Ni Kwamba Wakristo Wengi Hupanga Kama Ngazi Ule Utatu Wa Mungu. Tukijieleza Kwamaba Mungu Baba Ndio Mkuu, Kisha Yesu Alafu Roho Mtakatifu Akiwa Wa Watatu.

Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu, anayepasa kuabudiwa na kuheshimiwa. Baada ya miaka 20 ya huduma, nimeafikia jambo hili; umuhimu wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Kwa ufupi, nimeweza kuelewa, kutomuombea muumini yeyote kabla ya kumuita Roho Mtakatifu avunje vikwazo vyote kutoka kwa Shetani. Kila muumini lazima ajuwe pingamizi za Shetani kinyume na Ahadi za Mungu. Baada ya kumuita Roho Mtakatifu ndiposa naweza kuomba na yeyote yule ili Roho Mtakatifu afunguwe moyo wake aweze kupokea Upendo wa Mungu. Ningeliweza kunakili Neno chungu nzima, naweza kumuhurumia katika shida zake, na kufanya yote kuinuwa Roho yake. Lakini ni lazima yeye mwenyewe ajuwe Upendo na Amani ambayo Roho Mtakatifu pekee anaweza kumpatia.

2. Lazima Tuwe Na Hakika Kamili Kuwa Mungu Hu Bariki Wale Wamchao Bila Kusita.

“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.” (Waibrania 11:6). Mara nyingi tunasumbuka kushikilia Imani. Sote tunatamani Ahadi za Mungu, si kwa Amani yetu pekee lakini pia kumpendeza Mungu. Tunatamani Imani imtukuzayo Mungu. Kwa sababu hii, tunapata kusononeka maombi yetu yasipojibiwa. Tuanaanza kushuku Imani yetu, tukishangaa “je, uaminifu wangu kwa Mungu ni nadra sana? Je, niko mnyonge kuamini? Kwa nini mbingu zimefungwa juu yangu? Je, nimekwepa njia kidogo? Je, sija makinika ya kutosha? Je, kuna mizizi ya kutoamini ndani yangu? Tunajaribu sana kuamini, tuking’ang’ana kumpendeza Mungu na Imani kuu, mpaka tunazima Imani yetu kwa sababu ya hukumu tunayojitweka. Sasa, baada ya miaka 60 nikiwa katika huduma ya Mungu, nataka kuwaeleza Imani ya kamili ni nini kwangu:

  • Ni, kushikilia kamili Ahadi za Mungu pale ambapo hakuna kielelezo chochote kinachoonesha kutekelezwa kwa Ahadi hizo.
  • Ni, kumuamini Roho Mtakatifu kwa Utulivu wa Nafsi yangu, ni kiwa na hakika kwamba Mungu anayatenda yote na lengo la kunipatia mema
  • Ni, kukwamilia Ujumbe wa Paulo: “Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake. (Warumi 8:28).

Ujumbe maarufu wa Paulo kuhusu “katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja kwa mema” litajaribu Imani yetu tena na tena maisha yetu yote. Mara nyingi kwa macho ya kimwili, mambo yetu yanakaa kana kwamba yametumbukia nyongo. Walakini, katika majaribu yote, kuna kazi ya kweli ya milele inayoendelea pale. Mungu ayatenda yote pamoja kwa mpango wake juu yetu. Tunajuwa ilikuwa hivyo kwa Yosefu. Alipitia masaibu tele yaliokuwa shida tupu. Mpaka mwisho “Wakati Neno la Mungu lilipokuja (Zaburi 105:19). Mpaka wakati huwo, Neno la Mungu lilimjaribu. Je, unaweza basi kusema pamoja na Yosefu na Mtume Paulo “Yote yanafanya pamoja kwa mema? Je, Nafsi yako imetulizwa na ukweli huu, kwamba Mungu anafanya yote katika mpango kwa sababu yako? Unaamini kuwa katika uchungu wako – katika shida zako – katika upungufu wa ndoto zako, matumaini na malengo – Mungu alikuwa akiboresha undani wa imani yako kwake? Kwa Upendo wake, amekuwa akikuelekeza kwa Baraka, utakayopokea sasa na hata milele!

Mungu anatueleza katika Waibrania, “ni lazima uamini mimi ndimi Mbariki wako” tena muandishi asema, “Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi. (Waibrania 10:36).

Mungu haja Ahidi zaidi ya yale anayotaka kufanya. Abrahamu aliweza kuelewa haya tangu mwanzo wa Imani yake. Paulo asema, “Lakini Abrahamu hakusitasita kwa kutokuamini ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu, akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi. (Warumi 4:20–21).

Kwa Imani, Abrahamu “Alimtukuza Mungu”

Kama Abrahamu, tunamtukuza Mungu tunapoamini Ahadi zake zote. Pale mambo yote yanapokuwa sawa, ni rahisi kuwa na ushuhuda, “Mungu aweza kutenda yote!” tunaweza kueleza wengine kwamba Mungu atajibu maombi yao. Tunaweza kunena kuwa Mungu hutimiza Neno lake. Lakini mambo yanapoenda mrama kinyume na Ahadi za Mungu – pale vielelezo vyote vinakaa kama hukumu wala sio baraka – Roho Mtakatifu huinuka akiwa na Maneno halisi ya kutuliza. “Shikilia. Muamini! Hujatengwa na Upendo wa Mungu. Yuko kazini kila dakika ya Imani yako. Usitingisike. Bali, inuka na pigana vita vizuri vya Imani”

Nitawaaga na ujumbe huu maradufu kutoka kwa mtume Paulo. Anayetukumbusha Uaminifu wa Mungu katika kila hali, kila dakika ya maisha yetu.

“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga? Kama ilivyoandikwa : ‘‘Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.’’ Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda. 38Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, 39wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine cho chote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:35–39).

Amina!

Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)

Swahili