NANGA YA IMANI YETU

David Wilkerson (1931-2011)

Mstari mmoja wa Neno la Mungu utakuifazi kupitia nyakati yoyote na za hatari ikiwa utaukumbatiya kwa maisha yako yote. Mpendwa, karibisha mstari huu mmoja, uwuamini kabisa, na utakuwa chanzo cha nguvu za kila siku za imani yako:

"Basi msifane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba" (Mathayo 6:8).

Yesu anaandika mambo Baba yetu wa mbinguni anaeyajua kama tunayahitaji - kwa kifupi, chakula, kinywaji na nguo. "Kwa hiyo nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya maisha yenu, mtakula nini; wala juu ya mwili, mtavaa nini" (Luka 12:22). Mfumo wa msingi wa maisha yako unapaswa kuwa: Mungu anajua ... na hayo yote ni muhimu!

"Basi, ikiwa Mungu huvika majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa katika tanuri, Je! Hatawatendea ninyi Zaidi, enyi wenye kuwa na imani ndogo?" (12:28). Yesu anasema juu ya majani yaliokamili na yakiwa kijani leo, lakini yanakatwa kesho. Anatukumbusha kwamba aliiweka uhai na huduma na hatujali kufikiri yeye anajali mahitaji yetu kidogo. Ikiwa una wasiwasi juu ya ustawi wa familia yako, nina habari njema: watoto wako ni watoto wa Mungu na anajali kwa mpendwa wako zaidi kuliko wewe. Yesu anajua kile ambacho kila mmoja anachohitaji.

Yesu anajua kuhusu haja yako ya kuwa na paa juu ya kichwa chako; anajua kuhusu kodi yako au malipo ya mikopo kila mwezi. Anajua kuhusu mahitaji yako yote na unaweza kumwamini kikamilifu ili akutane na na hayo yote. Aliahidi kufanya hivyo!

Bwana anasema kwamba matajiri na maskini wote wako sawa, "Msiwe na wasiwasi juu ya mali zenu za kidunia. Nipe wakati bora na uniamini. Mimi nitajali mahitaji yako yote." "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa" (Mathayo 6:33).

Tiya imani yako kwa ukweli kwamba Baba yako wa mbinguni anajua yale unayohitaji. Anakufurahia sana wewe na ukiwa pamoja naye utakuwa salama salimini.