"NATAKA KUJUA MUNGU WAO"

Gary Wilkerson

"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanaume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenyewe nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani" (Isaya 9:6).

Wakati unabii wa kuzaliwa kwa Kristo ulikamilika, Mfalme Herode, mtawala wa Israeli, alitishiwa, kama ilivyokuwa kila mtu huko Yerusalemu (Mathayo 2:1-3). Inavyoonekana, walikuwa wanafurahia kwa kushikamana sana na dini yao iliyokufa, na hawakutaka mtu yeyote atetemeshe hali hiyo.

Vivyo hivyo ni kweli leo. Uadui unaoongezeka kuelekea ushahidi wa Krismasi yenyewe kwa njia nyingi: shule hazishiki tena sherehe za Krismasi; Maenosho ya Oli  ni marufuku katika maeneo ya umma; wafanyabiashara wakubwa manaita wateja wao kwa "Likizo Yenye Furaha" badala ya "Krismasi Njema," kwa kusema mfano mmoja kwa mifano michache tu. Yesu alitabiri kwamba siku ya kurudi kwake itakapokaribia "upendo wa wengi utapoa" (Mathayo 24:12), hivyo hii sio mshangao.

 Yesu alikuja ulimwenguni kuwa mwanga na hatupaswi kupoteza moyo wa Yesu kwa kuchukuliwa na vita vya utamaduni. Kama ulimwengu unavyozidi kudidimia chini zaidi, na malalamiko dhidi anatokea didhi ya chuki kubwa kwa Mwokozi wetu, basi mioyo yetu wenyewe itaongozwa na upendo wa Yesu Kristo. Na hebu ushuhuda wetu wa huruma na utakatifu kati ya kizazi cha uharibifu uwashituwe wale walio katika giza ili wageukiye nuru yake.

Kama kusudi la Krismasi linajaza mioyo yetu msimu huu, ninaomba kwamba wengi watatuangalia na kusema, "Nataka furaha na amani ninazoona katika watu hao. Lazima kuwe na kitu kwa ujumbe ambao wanatangaza na kuwaonyesha katika maisha yao. Ninataka kumjua Mungu wao."