NENO LENYE UHAI

Carter Conlon

Tunaishi katika siku za mwisho na ulimwengu kama tunavyojua unaenda ndani ya giza isiyoonekana. Unabii wa Kibiblia unaonekana mbele yetu kila siku, na hivi karibuni tutaona Yerusalemu iliyozingilwa na majeshi.

Yesu alionya kwamba katika siku za mwisho, manabii wengi wa uongo watatokea na Wakristo wengi watapotoshwa (tazama Mathayo 24:11). Hebu niwaambie kwa nini watapotoshwa: Ni rahisi tu, kwa sababu hawaishi katika Neno la Mungu! Wanafuata vitabu, mitindo, na wasemaji wenye kutania - lakini hawafungui maandiko ya Biblia.

Kumbuka, Biblia ni Neno lililo hai. "Kufafanusha maneno yako kwatia nuru" (Zaburi 119:130). "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. ... Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakingefanyika chochote kilichofanywa. ... Naye Neno aligeuka mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli" (Yohana 1:1, 3, 14). "Alikuja kwake, na wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wakugeuka watoto wa Mungu" (Yohana 1:11-12).

Neno la Mungu ni hai na nguvu ya kuumba na kurejesha moyo wa mwanadamu. Lina uwezo wa kutoa maono, uhuru, matumaini na nguvu. Na labda muhimu zaidi kwa wote katika kizazi hiki, Neno hutoa mwelekeo. Kutakuwa na mamilioni ya sauti za kuchanganya zilizotumwa na Jahannamu yenyewe, ili kuwapotosha watu wa Mungu na kuwatia mtego wavivu, lakini Mungu anaahidi kwamba Neno lake litakuwa taa ya miguu yetu na nuru kwa njia yetu (angalia Zaburi 119:105).

Carter Conlon alijiunga na  jopo la wachungaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji  muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa  kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.